Russia kujiondoa SWIFT ya Marekani na kujiunga na Sepam ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i69778-russia_kujiondoa_swift_ya_marekani_na_kujiunga_na_sepam_ya_iran
Russia imetangza kuwa itajiondoa katika mfumo wa kimataifa wa mabadilishano ya kifedha baina ya benki ujulikanao kama SWIFT na ambao unadhibitiwa na Marekani na badala yake itajiunga na mifumo mbadala ya kifedha ukiwemo ule mfumo wa kifedha wa Sepam wa Iran.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 04, 2021 21:50 UTC
  • Russia kujiondoa SWIFT ya Marekani na kujiunga na Sepam ya Iran

Russia imetangza kuwa itajiondoa katika mfumo wa kimataifa wa mabadilishano ya kifedha baina ya benki ujulikanao kama SWIFT na ambao unadhibitiwa na Marekani na badala yake itajiunga na mifumo mbadala ya kifedha ukiwemo ule mfumo wa kifedha wa Sepam wa Iran.

Akizungumza na Televisheni ya RT, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova amesema uamuzi huo umekuja baada ya Bunge la Ulaya kupitisha azimio la kutaka Russia itimuliwe katika mfumo wa kifedha wa SWIFT.

Amesema hivi sasa Russia inatafakari hatua za kuchukua iwapo azimio hilo litatekelezwa kivitendo na imeshapata njia za kuhakikisha kuwa haidhuriki endapo itatimuliwa katika mfumo huo wa kifedha wa nchi za Magharibi.

Amesema Russia inatafakri kutumia mifumo migine ya mabadilishano ya kifedha baina ya neno kama ule wa Iran ujulikanao kama Sepam na pia mifumo ya CUP na CIPS ya China.

Iran ilizindua mfumo wa Sepam mwezi Oktoba 2013 na imekuwa ikizihimiza nchi za Asia kuutumia badala ya kutegemea mfumo wa SWIFT.

Maria Zakharova

Mivutano baina ya Russia na Umoja wa Ulaya imeongezeka sana hivi sasa. Kuwekeana vikwazo viongozi wa kisiasa wa pande mbili ni silaha kuu inayotumiwa na pande hizo kuonesha ukubwa wa mivutano hiyo.

Ijapokuwa mivutano baina ya Umoja wa Ulaya na Russia iliongezeka mwaka 2014, hata hivyo mivutano hiyo imeongezeka vibaya mno tangu alipoingia madarakani rais mpya huko Marekani, Joe Biden.