Russia: Mazungumzo ya JCPOA yamefika marhala ya mwisho
https://parstoday.ir/sw/news/world-i71606-russia_mazungumzo_ya_jcpoa_yamefika_marhala_ya_mwisho
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na ambaye pia ni afisa wa ngazi ya juu katika timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Russia ametangaza kuwa, mazungumzo ya kuhuisha mapatano ya JCPOA yamefikia marhala ya mwisho.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 24, 2021 02:47 UTC
  • Russia: Mazungumzo ya JCPOA yamefika marhala ya mwisho

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na ambaye pia ni afisa wa ngazi ya juu katika timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Russia ametangaza kuwa, mazungumzo ya kuhuisha mapatano ya JCPOA yamefikia marhala ya mwisho.

Sergei Ryabakov amebainisha kuwa, tunaweza kusema kuwa tumefikia mstari wa mwisho wa mazungumzo ya JCPOA na maneno haya si kutia chumvi. Ryabakov alibainisha hayo jana katika kikao cha 25 cha mkutano wa kila mwaka wa Wawekezaji wa Russia.

Ameongeza kuwa, hatua ya mwisho ni hatua ngumu zaidi na kwamba maamuzi yote muhimu na ya muda mrefu yatachukuliwa katika miji mikuu ya nchi husika. Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Russia amesema, duru ya mwisho ya mazungumzo huenda ikafanyika Vienna iwapo pande husika katika mazungumzo zitaweza kutatua hitilafu zao. 

Sergei Ryabakov amesema ana matarajio na natija ya mazungumzo na anaamini kuwa mchakato huo utachukua wiki kadhaa tu na si miezi. Duru ya sita ya mazungumzo ya Vienna ya kuhuisha mapatano ya JCPOA ilimalizika Jumapili iliyopita kwa kufanyika kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA chini ya Mwenyekiti Enrique Mora Naibu Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya Anayehusika na Sera za Kigeni. Wakuu wa timu za mazungumzo wamesema wamefurahishwa na jitihada endelevu na kubwa za timu za wataalamu na kisha wakatathmini kwa pamoja matokeo ya mazungumzo  hayo.

Enrique Mora, Naibu Mjumbe wa EU sera za kigeni