Feb 02, 2022 08:09 UTC
  • Putin: Marekani inaitumia Ukraine kuidhibiti Russia

Rais wa Russia amesema kuwa Washington imejaribu kila iwezalo kuidhibiti Russia na inaitumia Ukraine kama wenzo wa kufanikisha lengo hilo.

Marekani na waitifaki wake wameibua mivutano katika eneo kwa kuiuzia Ukraine silaha mara kadhaa. Mwaka uliopita wa 2021 Marekani iliiuzia Ukraine silaha mara kadhaa khususan makombora ya kukabiliana na vifaru aina ya Javelin ili kuliimarisha jeshi la Ukraine dhidi ya Russia.  

Akihutubia jana, Rais Vladimir Putin ameashiria hali ya mivutano iliyojitokeza kati ya nchi yake na baadhi ya nchi za Magharibi na kusema: Marekani na muungano wa Nato zimepuuza wasiwasi wa Russia huku pande mbili hizo zikisisitiza tu juu ya nchi kuwa na haki ya kuchagua kuhusu usalama wao. Amesema, Russia inayachambua kwa karibu majibu ya Marekani na Nato kwa mapendekezo yake.  

Rais Putin ambaye alibainisha hayo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Viktor Orbán Waziri Mkuu wa Hungary amesisitiza kwa mara nyingine tena kuhusu takwa la Russia kwamba Nato haipasi kujipanua na kuelekea upande wa Mashariki.  

Ameongeza kuwa, Washington inataka kuiingiza vitani Russia ili kuiwekea vikwazo. Jumatatu wiki hii pia Dmitry Peskov Msemaji wa Rais wa Russia  aliitaka Marekani iache kushadidisha mivutano kandokando ya Ukraine. 

Dmitry Peskov, Msemaji wa Rais wa Russia 

 

Tags