Russia yatahadharisha juu ya uwezekano wa kupigana na Nato
https://parstoday.ir/sw/news/world-i82628-russia_yatahadharisha_juu_ya_uwezekano_wa_kupigana_na_nato
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetahadharisha juu ya uwezekano wa kujiri mapigano ya muda mrefu baina ya nchi hiyo na Shirika Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) katika katika eneo la Ncha ya Kaskazini.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 18, 2022 02:29 UTC
  • Russia yatahadharisha juu ya uwezekano wa kupigana na Nato

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetahadharisha juu ya uwezekano wa kujiri mapigano ya muda mrefu baina ya nchi hiyo na Shirika Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) katika katika eneo la Ncha ya Kaskazini.

Tokea Disemba mwaka jana Russia ilipotahadharisha kuhusu hatua za kujitanua za Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) iliwasilisha mapendekezo kadhaa kwa Marekani na sshirika hilo ikitaka kudhaminiwa usalama wake; hata hivyo pande mbili hizo zilikataa mapendekezo hayo. 

Nchi zisizo wanachama wa muungano wa NATO kama Finland na Sweden zinafikiria kujiunga na muungano huo tangu Russia ianzishe oparesheni ya kijeshi huko Ukraine baada ya upuuzaji wa nchi za Magharibi na Troika ya Ulaya kwa wasiwasi wa Moscow kuhusu usalama wake.

Vikosi vya muungano wa Nato 

Televisheni ya al Mayadeen pia jana Jumapili ilitangaza kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imeeleza kuwa, hatua ya Sweden na Finland ya kuomba kujiunga na NATO haitasaidia kuleta amani na hali ya kuaminiana katika eneo la Ncha ya Kaskazini.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imeongeza kuwa, kusimamishwa shughuli za Baraza la Ncha ya Kaskazini ni hatari kwa usalama wa eneo hilo na kwamba nchi za Magharibi haziwezi kudhamini ustawi endelevu katika eneo hiyo bila ya uwepo wa Russia.