Baadhi ya Waislamu waswali Iddi leo, wengine kuadhimisha sikukuu hii kesho
https://parstoday.ir/sw/news/world-i85638-baadhi_ya_waislamu_waswali_iddi_leo_wengine_kuadhimisha_sikukuu_hii_kesho
Baadhi ya Waislamu katika nchi kadhaa duniani wanaswali na kusherehekea sikukuu ya Idul Adh'ha hii leo, huku wengine wakitazamiwa kuadhimisha sherehe hizo kesho Jumapili.
(last modified 2025-10-20T07:03:11+00:00 )
Jul 09, 2022 04:09 UTC
  • Baadhi ya Waislamu waswali Iddi leo, wengine kuadhimisha sikukuu hii kesho

Baadhi ya Waislamu katika nchi kadhaa duniani wanaswali na kusherehekea sikukuu ya Idul Adh'ha hii leo, huku wengine wakitazamiwa kuadhimisha sherehe hizo kesho Jumapili.

Sikukuu hii ya Idul Hajj inaadhimishwa leo katika baadhi ya nchi na maeneo mengine ya dunia, sambamba na amali ya kuchinja wanyama na dhabihu inayofanyika huko katika ardhi tukufu ya Makka nchini Saudi Arabia.

Duru za habari zinaarifu kuwa, baadhi ya Waislamu wamesali na kuadhimisha sikukuu ya Iddul-Adh'ha hii leo katika nchi za Kenya na Uganda. Akthari ya Watanzania wanatazamiwa kuadhimisha siku hii tukufu kesho.

Kadhalika nchi za Kiislamu kama Iran na Indonesia zinatazamiwa kuadhimisha sikukuu hii adhimu ya Iddi ya kuchinja kesho Jumapili.

Hapo jana, Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia walisimama katika uwanja wa Arafa, kisimamo hicho kikiashiria kilele cha ibada tukufu ya Hijja. 

Redio Tehran inatoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa sikukuu hii kubwa.