Maelfu ya wakimbizi waokolewa katika Bahari ya Mediterranean
https://parstoday.ir/sw/news/world-i8863-maelfu_ya_wakimbizi_waokolewa_katika_bahari_ya_mediterranean
Gadi ya fukwe za bahari ya Italia imetangaza habari kwamba imewaokoa maelfu ya wakimbizi katika Bahari ya Mediterranean katika siku za Jumatano na Alkhamisi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 10, 2016 04:02 UTC
  • Maelfu ya wakimbizi waokolewa katika Bahari ya Mediterranean

Gadi ya fukwe za bahari ya Italia imetangaza habari kwamba imewaokoa maelfu ya wakimbizi katika Bahari ya Mediterranean katika siku za Jumatano na Alkhamisi.

Gazeti la Le Figaro la nchini Ufaransa limewanukuu askari hao wa kulinda fukwe za bahari wa nchini Italia wakisema jana kwamba, zaidi ya wakimbizi elfu tatu wameokolewa na askari hao katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita kwenye Bahari ya Mediterranean.

Gadi ya fukwe za baharini ya Italia imeongeza kuwa, viwiliwili viwili vya wakimbizi vimeopolewa baharini katika kipindi hicho cha masaa 48 yaliyopita.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, juzi Jumatano, wakimbizi 1100 na jana Alkhamisi wakimbizi wengine 1950 waliokolewa baharini na askari hao.

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya italia imesema kuwa, wakimbizi 50 elfu wameingia katika fukwe za Italia tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016 idadi ambayo imepungua kwa karibu asilimia 10 ikilinganishwa na muda kama huo mwaka jana.