Oct 18, 2022 07:37 UTC
  • Australia yatengua uamuzi wa kuitambua Quds kuwa mji mkuu wa Israel

Serikali ya Australia imetangaza habari ya kubatilisha uamuzi wake tata wa kulitambua eneo la magharibi mwa Quds linalokaliwa kwa mabavu, eti kuwa ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.

Katika kikao na waandishi wa habari Jumanne, Penny Wong, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia amesema serikali ya nchi hiyo inaunga mkono jitihada za kimataifa za kuitafuta suluhisho la kiuadilifu na la kudumu kadhia ya Palestina.

Wong amebainisha kuwa, hatima ya Quds inapaswa kuamuliwa kupitia mazungumzo baina ya Wapalestina na Waisraeli, na si kupitia uamuzi wa upande mmoja.

Disemba mwaka 2018, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison alisema, nchi hiyo sasa inalitambua eneo la magharibi mwa Quds ambayo ni makao makuu ya Bunge la Israel (Knesset) na taasisi nyingi za serikali, kama eti mji mkuu wa Israel.

Ubalozi wa Marekani mjini Quds

Alichukua uamuzi huo mwaka mmoja baada ya aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza Quds kuwa eti mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel; na Mei 14 mwaka uliofuata, Washington ikauhamishia ubalozi wake katika mji huo wa Waislamu kutoka Tel Aviv.

Hata hivyo Penny Wong, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia amesema hii leo kuwa, "Nasikitika kuwa uamuzi wa Bwana Harrison kutanguliza siasa ulipelekea Australia kubadili msimamo wake, na uamuzi huo umewaathiri watu wengi katika jamii ya Australia ambao wanalichukuliwa kwa uzito mkubwa suala hili."

Tags