Nov 28, 2022 11:22 UTC
  • Trump aibua tuhuma nzito: Wizara ya Sheria ya Marekani ni fisadi

Rais wa zamani wa Marekani ameishutumu Wizara ya Sheria ya nchi hiyo kwa ufisadi na kwa kumhusisha yeye na mashtaka yasiyo ya haki.

Donald Trump ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social: "wizara ya sheria ni fisadi na imemlipa Christopher Steele, jasusi wa zamani wa Uingereza, dola milioni moja ili aseme uongo kuhusu mimi".
Kitambo nyuma, mahakama nchini Marekani ilimtoa hatiani mchambuzi wa Kirussia Igor Donchenko aliyeshtakiwa kwa tuhuma za kusema uwongo katika kesi ya kula njama Trump kwa kushirikiana na Russia. Katika kauli aliyotoa mwezi uliopita kuhusiana habari hiyo, Trump alisema, hatua hiyo inadhihirisha sura halisi ya kuaibisha ya mfumo wa mahakama wa Marekani.
Jasusi wa zamani wa Uingereza Steele alikuwa ametayarisha ripoti kuhusu Trump ambayo ilifichuliwa kwa vyombo vya habari na FBI. Katika ripoti hiyo, Steele alikuwa ametoa maelezo kuhusu jinsi Warussia walivyomsaidia Trump kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2016.
Christopher Steele

Waendesha mashtaka walikuwa wamemshutumu Donchenko kwa kudanganya kuhusu vyanzo vilivyompatia taarifa Steele, lakini mchambuzi huyo wa Kirusi alikana shtaka hilo na akafutiwa mashtaka.

Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi uliopita wa Oktoba, mchambuzi Mwandamizi wa FBI Brian Auten alitoa ushahidi mahakamani kwamba FBI ilimlipa Steele dola milioni moja ili atoe ushahidi wa kuthibitisha madai yake ya kula njama Trump kwa kushirikiana na Russia.
Maafisa wa Russia walikanusha shutuma zilizotolewa na maafisa wa Marekani za kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.
Katika miaka ya karibuni uhusiano wa Moscow na Washington umeharibika na kugubikwa na mikwaruzano mikubwa kutokana na masuala kadhaa ikiwemo kupanuliwa satua na ushawishi wa kijeshi wa shirika la kijeshi la NATO na zaidi Marekani karibu na hata kwenye nchi zinazopakana na Russia huko Ulaya Mashariki, madai kwamba Russia imeingilia uchaguzi wa Marekani, kadhia ya kiongozi wa upinzani nchini Russia Alexei Navalny, vikwazo vya upande mmoja vya Washington dhidi ya Moscow pamoja na mgogoro wa Ukraine na ule wa Peninsula ya Crimea.../

Tags