May 24, 2023 10:50 UTC

Rais wa Russia ameeleza kuwa katika hali ambayo Wamagharibi wanalenga kuzidisha hali ya wasiwasi na ukosefu wa usalama duniani; nchi huru kuanzia Asia hadi Afrika zinapaswa kusaidia katika usanifu usiogawanyika wa usalama duniani.

Rais Vladmir Putin amesema katika ujumbe wake uliotumwa kwa njia ya video kwa viongozi wa ngazi za juu wa usalama wa nchi zaidi ya mia moja wanaoshiriki Mkutano wa 11 wa Usalama Duniani huko Moscow kwamba: Njia mbadala zaidi kwa sera na vitisho haribifu vya nchi za Magharibi ni kuimarisha usalama na amani duniani na kuwa na mfumo mmoja usiogawanyika wa usalama katika ulimwengu wa sasa. 

Rais wa Russia aidha amesisitiza kuwa tuna ulimwengu wa kambi kadhaa na wa kiadilifu na kwamba, fikra za Kinazi na za kuchupa mipaka hatimaye zitalazimika kujiunga na historia." 

Mkutano wa 15 wa Usalama Duniani unaohudhuriwa na Viongozi wa Ngazi ya juu kutoka nchi  zaidi ya miaka moja umeanza leo huko Moscow mji mkuu wa Russia kwa kuhudhuriwa na Makatibu wa Mabaraza ya Usalama wa Taifa, Washauri wa Marais wa Nchi katika Masuala ya Usalama wa Taifa, Makamanda wa Vitengo Maalumu na Vyombo vya Kutekeleza Sheria kutoka nchi 101 duniani.  

Mkutano wa 15 wa Usalama Duniani mjini Moscow 

Sambamba na kufanyika kikao cha pamoja na kamati maalumu; Mkutano wa 15 wa Usalama Duniani unaofanyika mara moja kwa mwaka umekuwa mahali pa mashauriano na mazungumzo baina ya pande mbili na pande kadhaa kati ya viongozi washiriki.

Tags