-
Kombe ya Dunia: Morocco yaandika historia; timu ya kwanza ya Afrika kutinga nusu fainali
Dec 11, 2022 14:46Timu ya soka ya taifa ya Morocco imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kusonga mbele katika nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ureno na kumuacha gwiji wa soka Cristiano Ronald na wenzake wakigaragara kwa vilio na majonzi.
-
Kandanda: Croatia na Argentina zatinga nusu fainali ya Kombe la Dunia
Dec 10, 2022 11:02Timu za taifa za soka za Croatia na Argentina zimetinga hatua ya nusu fainali ya michuano yasoka ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar baada ya kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili za kwanza za robo fainali.
-
Hizbullah yaipongeza timu ya soka ya Morocco kwa kuinyuka Uhispania na kuinua bendera ya Palestina
Dec 07, 2022 13:52Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa "Twitter" ambapo ameipongeza Morocco kwa ushindi wa timu ya kandanda ya nchi hiyo dhidi ya Uhispania hiyo jana na kufuzu kuingia robo fainali ya mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar.
-
Morroco yaigaragaza Uhispania na kujiandikia historia ya Kombe la Dunia
Dec 07, 2022 13:38Timu ya taifa ya soka ya Morocco imepata ushindi mkubwa kwa kuwaondoa Uhispania kwa mikwaju ya penalti baada ya kutaka sare ya kutofungana.
-
Ripoti: Harakati ya kutetea ushoga iliibua tatizo kubwa ndani ya timu ya taifa ya Ujerumani huko Qatar
Dec 07, 2022 03:12Harakati ya "kuziba midomo" iliyofanywa na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Ujerumani kwenye mechi yao ya ufunguzi katika Kombe la Dunia 2022 huko Qatar dhidi ya Japan, ilisababisha matatizo ndani ya kambi ya timu hiyo, na kuibua tofauti kati ya wachezaji ambao walikataa kushiriki kwenye kampeni ya kutetea ushoga.
-
Palestina yaendelea kuungwa mkono katika mashindano ya Kombe la Dunia, Qatar
Dec 06, 2022 07:49Moja ya matukio yenye kuvutia katika mashindano ya Soka ya Kombe la Dunia huko Qatar ni kitendo cha watazamaji kutoka nchi mbalimbali kuiunga mkono Palestina mkabala wa utawala wa Kizayuni.
-
Kombe la Dunia; mwanajeshi Mzayuni akimbia haraka Qatar baada ya kugunduliwa uhakika wake
Dec 04, 2022 11:41Mwanajeshi mmoja Mzayuni aliyejipenyeza nchini Qatar kwa sura bandia ya msanii wa vichekesho, amekimbia haraka nchini humo baada ya Mpalestina mmoja kumgundua na kufichua uhakika wake kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
-
Kombe la Dunia Qatar limeonyesha kufeli mpango wa kuanzisha uhusiano na Israel
Dec 04, 2022 02:38Khatibu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa huko Palestina amesema, wananchi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu wanaoshuhudia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar wamethibitisha kugonga mwamba mpango mchafu wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.
-
Cameroon, timu ya kwanza ya Afrika kuishinda Brazil, Ghana yalipiza kisasi kwa Uruguay
Dec 03, 2022 04:19Timu ya Taifa ya Cameroon imeweka historia ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kuwahi kuishinda Timu ya Taifa ya Brazil katika mashindano ya Kombe la Dunia, baada ya kumchabanga mwamba huyo wa soka wa Amerika ya Latini bao 1-0 katika hatua ya awali ya Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yanayoendelea hivi sasa nchini Qatar.
-
Sheikh Ali Da'mush: Mshindi halisi wa Kombe la Dunia Qatar ni Palestina
Dec 03, 2022 02:21Naibu wa Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mshindi halisi wa fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar ni taifa la Palestina kutokana na wimbi kubwa la wachezaji na mashabiki wa soka kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.