Dec 31, 2024 02:41 UTC
  • Jumanne tarehe 31 Disemba 2024

Leo ni Jumanne tarehe 29 Mfunguo Tisa Jamadithani 1446 Hijria sawa na tarehe 31 Disemba 2024.

Tarehe 31 Disemba miaka 510 iliyopita Andreas Vesalius, daktari na mpasuaji maarufu wa Ubelgiji, alizaliwa huko Brussels, mji mkuu wa nchi hiyo. 

Umaarufu wake unatokana na juhudi zake za kuelewa kazi ya viungo mbalimbali vya mwili kupitia upasuaji wa viungo hivyo. Kwa sababu hii, Vesalius ameitwa baba wa sayansi ya anatomia, na kitabu chake kiitwacho "Kiwanda cha Mwili wa Binadamu" (The Factory of the Human Body) pia kinazungumzia maudhuui hii. aliaga dunia mwaka 1564.   

Andreas Vesalius

Katika siku kama ya leo miaka 197 iliyopita, yaani tarehe 31 Disemba mwaka 1827 kibiriti kilivumbuliwa na John Walker mtaalamu wa madawa wa Uingereza.

Hata hivyo awali, mbali na kibiriti cha Walker kuwaka kwa taabu na mashaka kilikuwa pia na hatari kwa watumiaji wake. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana wataalamu wengine wakafanya jitihada za kukikamilisha kibiriti hicho.

Hatimaye mwaka 1855 mtaalamu mmoja wa Kiswedeni alifanikiwa kutengeneza kibiriti kama hiki kinachotumiwa leo hii baada ya kufanya majaribio na utafiti wa muda mrefu.   ****

Miaka 149 iliyopita katika siku kama ya leo Arthur Christensen mtaalamu wa masuala ya Mashariki alizaliwa huko Copenhagen mji mkuu wa Denmark.

Christensen alionyesha hamu kubwa ya kujifunza masuala ya Mashariki hususan historia ya Iran na mwishoni mwa masomo yake, alifanya utafiti kuhusu historia ya fasihi ya Irani.

Arthur Christensen aliweza kujifunza vyema lugha ya Kifarsi. Mojawapo ya vitabu vyake muhimu ni kile alichokipa jina la "Iran katika Zama za Wasasani." Christensen aliaga dunia mwaka 1945.   

Arthur Christensen

Katika siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, Rais Boris Yeltsin wa Russia aliondoka madarakani na nafasi yake ikachukuliwa na Vladimir Putin.

Kipindi fulani Yeltsin alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti. Boris Yeltsin alichaguliwa kuwa Rais wa Russia Januari mwaka 1991 na alikuwa akiungwa mkono na madola ya Magharibi. Hata baada ya kusambaratika Umoja wa Sovieti mwishoni mwa mwaka 1991, aliendelea kuwa Rais wa Russia akitumai kwamba, kwa kutumia misaada ya kifedha ya Magharibi angeweza kuiokoa nchi hiyo kutokana na matatizo ya kiuchumi yake ya kiuchumi.

Kinyume na matarajio yake, viongozi wa madola ya Magharibi hawakutekeleza ahadi zao, hali iliyopelekea siasa za Rais Boris Yeltsin kushindwa.

Kushambuliwa kijeshi eneo lililotangaza kujitawala la Chechnia na kukaliwa kwa mabavu ardhi hiyo na majeshi ya Russia, ni miongoni mwa matukio yaliyojiri katika kipindi cha utawala wa Boris Yeltsin nchini Russia.

Rais Boris Yeltsin