Jumanne, tarehe 06 Januari, 2026
-
Leo Katika Historia
Leo ni Jumanne tarehe 16 Rajab 1447 Hijria sawa na Januari 06 mwaka 2026.
Miaka 908 iliyopita siku hii ya leo, 16 Rajab 539 Hijria, Ibn Khairun, msomi maarufu wa Hadithi alifariki dunia.
Abu Mansur Muhammad ibn Abdul Malik ibn Hassan ibn Ibrahim Attar, anayejulikana kama Ibn Khayrun, alizaliwa Baghdad mwaka wa 454 Hijria, katika familia ya wasomi wa Hadithi na qiraa ya Qur'ani. Alijifunza elimu ya qiraa kwa masheikh maarufu wa mji wake, kama vile Abul-Barakat na Abdul-Sayyid. Miongoni mwa kazi zake ni Al-Miftah na Al-Muwwadh, ambazo vinavyojadili visomo kumi vyua Qur'ani.
Ibn Khairun alifariki duniia huko Baghdad tarehe 16 Rajab, 539 Hijria, akiwa na umri wa miaka 85.

Siku kama ya leo 165 iliyopita ilianzishwa nchi ya Romania. Mpango wa kuasisiwa nchi ya Romania ulibuniwa tarehe 13 Disemba 1859 kwa kuunganishwa miji miwili midogo ya Moldavia na Wallachia.
Miaka miwili baadaye majimbo na miji mingine ilijiunga na umoja huo na kuundwa nchi ya Romania. ***
Katika siku kama ya leo miaka 107 iliyopita, Theodore Roosevelt, Rais wa zamani wa Marekani aliaga dunia.
Alizaliwa Oktoba 27 mwaka 1857 na alikuwa Rais wa 26 wa Marekani. Alianza kujihusisha na harakati za kisiasa akiwa katika rika la ujana na baada ya kuwa mwanachama wa chama wa Repulican aliteuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho. AQlichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 1901. Katika mwaka wake wa kwanza madarakani, Roosevelt aliimarisha uwepo wa jeshi la Marekani huko Cuba, ambayo ilikuwa imevamiwa na kudhibitiwa na marekani. Wakati huo ndipo kilipoanzishwa kituo kikubwa cha jeshi la majini la Marekani huko Cuba, kinachojulikana kama Guantanamo.
Miongoni mwa matukio muhimu ya kipindi cha utawala wa Roosevelt ni pamoja na kujitenga Panama kutoka Colombia na kuanza ujenzi wa Mfereji wa Panama. Tukio jingine muhimu la zama za Roosevelt ni kuharibiwa kikamilifu mji wa San Francisco kutokana na tetemeko kubwa la ardhi.
Katika siku kama ya leo miaka 66 iliyopita alifariki dunia Ali Isfandiyari mashuhuri kwa jina la Nima Yushij mwasisi wa mashairi ya kisasa nchini Iran.
Isfandiyari alizaliwa katika mojawapo ya vijiji vya mkoa wa Mazandaran kwa jina la Yush huko kaskazini mwa Iran. Malenga huyo baadaye alielekea Tehran na kuanza kujifunza lugha ya Kifaransa. Nima Yushij alianza kutunga mashairi na kubuni mfumo mpya wa mashairi.
Miongoni mwa sifa za mfumo huo wa mashairi mapya ni kueleza masuala ya jamii kwa lugha nyepesi na kutokuwa na wizani. Kazi muhimu zaidi ya malenga huyo mashuhuri wa Iran ni maarufu kwa jina la "Afsaneh".
Siku kama ya leo miaka 45 iliyopita kulitokea hamasa ya mashahidi wa Hoveyzeh iliyoongozwa na Shahidi Alamul Huda katika miezi ya mwanzoni mwa uvamizi wa Iraq dhidi ya ardhi ya Iran.
Mwezi Dei mwaka 1359 Hijria Shamsia na baada ya jeshi la Iran ya Kiislamu kuvishinda vikosi zaidi ya viwili vya jeshi la Iraq huko kusini mwa eneo la Susangerd, kundi moja la Jeshi la Sepah la Ahvaz huko kusini mwa Iran lilitumwa katika mji wa Hoveyzeh kwenda kuulinda mji huo mbele ya mashambulizi ya Iraq. Hata hivyo kutokana na kuchelewa kufika zana na hujuma kubwa ya Iraq, jeshi la Iran lililazimika kurudi nyuma. Wakati huo zaidi ya wapiganaji mia moja wa Jeshi la Sepah, wapiganaji wa kujitolea na wanafunzi wa vyuo vikuu wafuasi waaminifu wa Imam Khomeini wakiongozwa na Sayyid Muhammad Hussein Alamul Huda walibakia katika mji huo wa Hoveyzeh wakipambana na adui na wakauawa shahidi.
Baadaye jeshi la Iraq liliuvunja kabisa mji wa Hoveyzeh na kuusawazisha na ardhi. Pamoja na hayo ushujaa wa vijana hao shupavu wa Iran waliosabilia roho zao kulinda ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu umebakia hai katika historia ya Iran.