Nov 03, 2017 04:08 UTC
  • Ijumaa, Novemba 3, 2017

Leo ni Ijumaa tarehe 14 Mfunguo Tano Safar 1439 Hijria sawa na Novemba 3, 2017 Milaadia.

siku kama ya leo miaka 807 iliyopita sawa na tarehe 14 Safar mwaka 632 Hijria alifariki dunia Abul Mahasin Bahauddin mashuhuri kwa jina la Ibn Shidad, fakihi, kadhi na mwanahistoria wa Kiislamu. Alizaliwa mwaka 539 huko Mosul, moja ya miji ya Iraq na alihifadhi Qur'ani akiwa bado mtoto na baadaye akajifunza hadithi, tafsiri na kusoma Qur'ani na kupata umahiri mkubwa katika taaluma hizo. Ibn Shidad alifanya safari katika nchi mbalimbali za Kiislamu kwa ajili ya kutafuta elimu. Miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri ni an Nawadir al Sultwaniya, Dalailul Ah-kam na al Aswaa kinachozungumzia maisha ya Nabii Musa A.S. na mapambano yake dhidi ya Firauni.

ا

Miaka 432 iliyopita katika siku kama hii ya leo alizaliwa Mulla Muhsin Faidh Kashani, aliyekuwa faqihi, mpokezi wa hadithi, mwanafalsafa na arifu mkubwa wa Kiislamu nchini Iran. Faidh Kashani alipata elimu za fiqhi, hadithi, tafsiri na falsafa kwa wanazuoni wakubwa wa zama zake kama Muhammad Taqi Majlisi, Sheikh Bahai na Mulla Sadra. Msomi huyo mkubwa ameandika vitabu vingi, mashuhuri zaidi vikiwa ni tafsiri ya Qur'ani ya al Swafi, Mafatiihu Sharaai', al Wafi na al Muhajjatul Baidhaa.

Kaburi la Faidh Kashani katika mji wa Kashan, Iran

Siku kama ya leo miaka 114 iliyopita mwafaka na leo Panama ilifanikiwa kujipatia uhuru wake kutoka Colombia na siku kama hii huadhimishwa nchini humo kamasiku ya taifa. Ardhi ya Panama iligunduliwa na kukaliwa kwa mabavu na Wahispania mnamo mwaka 1501 Miladia.Panama ilikaliwa kwa mabavu na Colombia mwaka 1821 Miladia na tangu wakati huo wananchi wa nchi hiyo walianzisha mapambano dhidi ya wavamizi wa Colombia. Mapambano hayo ya wananchi yalishadidi zaidi baada ya kuwasilishwa mpango wa mfereji wa Panama. Mwaka 1903,Panama ikafanikiwa kujitenga na Colombiana kujitawala. 

Bendera ya Panama

Siku kama ya leo miaka 61 iliyopita wakati wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Misri, askari wa utawala huo waliwaua kwa umati Wapalestina katika mji wa Khan Yunus uliopo katika Ukanda wa Gaza. Baada ya kuingia katika mji huo askari hao wa Kizayuni waliwaua askari 25 wa Misri na baadaye wakavamia hospitali na kuwaua wagonjwa na wauguzi waliokuwa humo. Baadaye askari hao katili wa utawala wa Kizayuni walishambulia kwa mabomu na kuteketeza kambi ya wakimbizi ya mji wa Khan Yunus ambako makumi ya wanawake na watoto wadogo walikuwa wakiishi.

Eneo la Khan Yunis, Ukanda wa Gaza

Siku kama hii ya leo miaka 44 iliyopita inayosadifiana na tarehe 12 Aban 1352 Hijria Shamsia, alifariki dunia Ayatullah Mirza Abul Hussan Shaarani arifu, faqihi na msomi mkubwa wa Kiislamu akiwa na umri wa miaka 71. Msomi huyo alibobea katika elimu mbalimbali za kidini na alikuwa mahiri katika lugha kadhaa za kigeni. Msomi huyo ameandika vitabu vingi na alikuwa mahiri katika elimu za mujumu na nyota.

Ayatullah Mirza Abul Hussan Shaarani

Na siku kama ya leo miaka 21 iliyopita, alifariki dunia Jenerali Jean-Bedel Bokassa dikteta wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bokassa alichukua madaraka mwaka 1921 kupitia mapinduzi ya kijeshi, baada ya kuiondoa madarakani serikali ya Rais David Dacko kwa uungaji mkono wa Ufaransa. Katika miaka 14 ya utawala wake, kiongozi huyo alitenda jinai na mauaji mbalimbali na kujilimbikizia mali nyingi.

Jean-Bédel Bokassa

 

Tags