May 18, 2018 02:39 UTC
  • Ijumaa, Mei 18, 2018

Leo ni Ijumaa, tarehe Pili Ramadhani mwaka 1439 Hijria, inayosadifiana na tarehe 18 Mei, mwaka 2018 Miladia.

Siku hii ya leo kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, yaani tarehe 28 Ordibehesht ni siku ya kumuenzi mwansayansi mkubwa, mshairi na msomi mtajika wa Irfan wa Iran, aliyefahamika kwa jina Hakim Omar Khayyam. Abul Fatah Omar ibn Ibrahim Khayyam Neishabouri, mwanafalsafa, mwanahesabati, mnajimu, mshairi, tabibu na mnajimu mkubwa wa Kiirani alizaliwa mwishoni mwa karne ya 5 au mwanzoni mwa karne ya 6 Hijria. Alizaliwa kati ya mwaka 417 na 440, katika mji wa Neishabour, katika mkoa wa Razavi Khorasan kaskazini mashariki mwa Iran. Katika uhai wake, Khayyam alipata umashuhuri kutokana na busara na kipaji kikubwa alichokuwa nacho katika nyuga za utabibu, unajimu na hesabati, lakini dunia ya leo inamkubuka kuwa bingwa wa falsafa. Kitabu chake mashuhuri alichokipa jina la Ru'ba'iyat  kinatambulika kote duniani, na kimetarjumiwa kwa lugha nyingi mashuhuri. Miongoni mwa kazi zake nyingine ni vitabu vya Nowruznome na Risala ya Mazingira.

XXXXXXXXXX

Miaka 214 iliyopita katika siku kama ya leo, yaani tarehe 18 Mei mwaka 1804 Miladia, kwa idhini ya Bunge la Seneti la Ufaransa, Napoleone Bonaparte alitangazwa kuwa mfalme wa Ufaransa na kwa utaratibu huo kwa mara nyingine tena utawala wa kifalme ukatawala nchini humo kwa miaka 15. Hata hivyo, mfumo wa kifalme ulifikia mwisho miaka kumi baadaye, sawa na tarehe 11 Aprili mwaka 1814, baada ya Napoleone Bonaparte kushindwa katika vita vyake na nchi za Ulaya na kubaidishwa.

ناپلئون بناپارت

XXXXXXXXXX

Miaka 188 iliyopita, sawa na tarehe 18 Mei maka 1830 Miladia, jeshi la Ufaransa lilianzisha operesheni ya kuikalia kwa mabavu Algeria. Kisingizio cha Charles wa Kumi mfalme dikteta wa wakati huo wa Ufaransa cha kutoa amri ya kufanywa  mashambulio hayo, ilikuwa sababu ya hujuma hiyo kufuatia vitisho vilivyokuwa vimetolewa miaka mitatu kabla na mtawala wa wakati huo wa Algeria akiitaka Ufaransa ilipe deni la nchi hiyo la Franc milioni saba. Hata hivyo, kinyume na ilivyodhania Paris, wananchi wa Algeria walisimama kidete katika kukabiliana na mashambulio hayo. Ijapokuwa Ufaransa ilifanikiwa kuikalia kwa mabavu Algeria na kupora maliasili na utajiri wa nchi hiyo, hatimaye nchi hiyo ya Kiafrika ilijipatia uhuru wake mwaka 1962.

پرچم  الجزایر

XXXXXXXXXXX

Na siku kama ya leo miaka 44 iliyopita, nchi ya India ilifanya jaribio la kwanza la nyuklia katika jangwa la Rajasthan magharibi mwa nchi hiyo na jirani na mpaka wake na Pakistan. Kwa utaratibu huo, India nayo ikawa nchi ya sita baada ya Marekani, Umoja wa Kisovieti, Ufaransa, Uingereza na China katika uwanja huo wa nyuklia. Miaka 24 baadaye yaani mwaka 1998 India ilifanya majaribio mengine matano ya nyuklia na kufanikiwa kutengeneza silaha za atomiki.

آزمایش هسته ای 

 

 

  

 

 

Tags