Feb 12, 2019 22:59 UTC
  • Jumatano tarehe 13 Februari 2019

Leo ni Jumatano tarehe 7 Jamadithani 1440 Hijria sawa na tarehe 13 Februari 2019.

 Siku kama ya leo miaka 915 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, alinyongwa na kuuliwa shahidi arifu mkubwa wa Kiislamu Ainul Qudhat Hamedani, aliyekuwa na lakabu ya Abul Fadhaail. Alikuwa fakihi, mwanafasihi, msomi, mshairi na malenga stadi. Ainul Qudhat alizaliwa mwaka 492 Hijria. Msomi huyo hakuwa na woga katika kueleza itikadi zake na alikuwa shujaa na muwazi. Kutokana na sifa hiyo mwaka 525 Hijria alikamatwa kwa amri ya waziri wa Sultani Ahmad Sanjar wa utawala wa Kiseljuqi na kufungwa mjini Baghdad. Baadaye alihamishiwa Hamedan nchini Iran na kunyongwa kandokando ya shule yake. Miongoni mwa vitabu vya Ainul Qudhat Hamedani ni "Tamhidaat" na "Haqaiqul Qur'an."

Ainul Qudhat Hamedani

Katika siku kama ya leo miaka 330 iliyopita tangazo lililojulikana kama Tangazo la Sheria lilisomwa katika sherehe za kumvika taji Mfalme William wa Tatu na Malkia Marry wa Pili wa Uingereza na kuanzia hapo mfumo wa utawala wa nchi hiyo ukabadilika na kuwa utawala wa kifalme wa kikatiba. Kwa mujibu wa tangazo hilo, madaraka ya Mfalme wa Uingereza yalipunguzwa na kukabidhiwa bunge la nchi hiyo.

 

Na miaka 31 iliyopita katika siku kama hii ya leo, aliaga dunia Ayatullah Sheikh Salman Khaqani. Alizaliwa mwaka 1293 Hijria Shamsia katika moja ya miji ya kusini mwa Iraq ya leo. Baada ya kupitisha kipindi cha utoto, akiwa na umri wa miaka 13 alihajiri na kuelekea Najaf al-Ashraf kwa ajili ya kupata masomo ya dini. Akiendelea na masomo yake, Sheikh Salman Khaqani hakuacha kujihusisha na harakati za kijamii, kiasiasa na kifasihi. Akiwa na umri wa miaka 43 na baada ya kufariki dunia baba yake aliyekuwa mmoja wa maulama wa Khorramshahr hapa Iran, aliuchagua mji huo kuwa makazi yake. Katika kipindi cha miongo mitatu ya kuishi kwake mjini Khorramshahr, mwanazuoni huyo alijishughulisha na kuongoza wananchi na kutoa huduma zenye thamani kubwa. Baada ya kuanza vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa Baath wa Iraq, nyumba ya alimu huyo ilikuwa kimbilio la watu hadi iliposhambulkiwa na kuhatribiwa. Hatimaye mwanazuoni huyo mchamungu aliaga dunia mjini Qum katika siku kama hii ya leo akiwa na umri wa miaka 76. 

Ayatullah Sheikh Salman Khaqani