May 06, 2019 03:26 UTC
  • Jumatatu, Mei 6, 2019

Leo ni Jumatatu tarehe 30 Shaaban mwaka 1440 Hijria mwafaka na tarehe Mei 6 2019 Milaadia.

Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita, alizaliwa Czechoslovakia, Sigmund Freud daktari wa magonjwa ya akili na raia wa Austria. Akiwa na umri wa miaka minne alihamia mjini Vienna akiwa na wazazi wake. Aidha alipofikisha umri wa miaka saba alijiandikisha katika chuo kidogo cha udaktari ambapo akiwa na miaka 29 alitokea kuwa tabibu aliyebobea kutibu magonjwa ya akili. Baada ya kutibu wagonjwa kadhaa wenye matatizo hayo alipata uzoefu mkubwa suala ambalo lilimsukuma kufanya majaribio kadhaa katika uga huo. Daktari huyo alifanya utafiti na kutwalii matatizo mbalimbali ya kiakili yanayomkumba binadamu na kutoa maoni na nadharia mpya kuhusu chanzo cha magonjwa ya akili. Kwa ajili hiyo anahesabiwa kuwa mwasisi wa elimu ya uchunguzi wa kisaikolojia au Psychoanalysis. Sigmund Freud alifariki dunia tarehe 23 Septemba 1939 akiwa na umri wa miaka 83 baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Sigmund Freud

 

Siku kama ya leo miaka 70 iliyopita yaani tarehe 6 Mei alifariki dunia Maurice Maeterlinck tabibu na mwandishi wa Kibelgiji akiwa na umri wa miaka 87. Alihitimu shahada ya sheria na baadaye akajishughulisha na masuala ya uwakili. Hata hivyo kwa kuzingatia kuwa hakupenda sana taaluma ya sheria, Maurice alielekea Paris, Ufaransa na kuanza kujishughulisha na masuala ya uandishi. Mwandishi huyo wa Kifaransa ameacha athari nyingi zenye thamani na aliandika tamthiliya aliyoiita 'Ndege wa Bluu', iliyofasiriwa katika lugha mbalimbali za dunia.

Maurice Maeterlinck

 

Siku kama ya leo miaka 160 iliyopita alifariki dunia mtaalamu wa masuala ya kimaumbile na msomi mkubwa wa Kijerumani Alexander Humboldt. Alizaliwa mwaka 1769 huko Berlin, Ujerumani. Alifanya safari ndefu katika mabara ya Asia na Amerika kwa ajili ya kufanya utafiti. Tafiti nyingi za msomi huyo zilihusu namna dunia ilivyoumbwa.

Alexander Humboldt

 

Siku kama ya leo miaka 137 iliyopita yaani tarehe 6 Mei 1882, kulitangazwa habari ya mafanikio ya kugunduliwa vijidudu maradhi vya ugonjwa wa kifua kikuu na Robert Koch. Wiki mbili kabla ya hapo, mtaalamu huyo wa masuala ya baiolojia alikuwa amegundua vijidudu maradhi hivyo ambavyo vilikuwa vimeua zaidi ya watu bilioni moja katika kipindi chote cha historia. Baadaye Prof. Robert Koch aligundua njia ya kufubaza na kutenga vijidudu maradhi hivyo ambavyo vilikuwa sugu mkabala wa dawa na vilikuwa na uwezo wa kujificha mwilini kwa miaka mingi na kisha kujitokeza baadaye. Mbali na kugundua vijidudu maradhi vya kifua kikuu, Prof. Robert Koch pia aligundua vijidudu maradhi vya kipindupindu katika safari zake katika nchi za Misri na India na mwaka 1906 alitengeneza dawa ya Atoxy inayoshabihiana na Quinine. Prof. Robert Koch anatambuliwa kuwa mtaalamu mkubwa zaidi wa vijidudu maradhi duniani baada ya Luis Pastore na alitoa huduma kubwa sana kwa elimu na sayansi ambayo kamwe haitasahaulika.

Robert Koch