Jul 29, 2019 04:16 UTC
  • Jumatatu, 29 Julai, 2019

Leo ni Jumatatu tarehe 26 Dhulqaada 1440 Hijria swa na Julai 29 mwaka 2019

Siku kama ya leo miaka 38 iliyopita Abul Hassan Bani Sadr, rais aliyeuzuliwa wa Iran alikimbia nchi akiwa pamoja na kiongozi wa kundi la Munafiqin la MKO, Mas'ud Rajavi. Siku 37 kabla yake Bani Sadr alikuwa ameuzuliwa cheo cha rais kutokana na kukosa ustahiki, kuzusha machafuko nchini na kushindwa kulinda nchi mbele ya hujuma za utawala wa Saddam Hussein. Bani Sadr alikuwa na matumaini kwamba, mauaji ya kinyama yaliyokuwa yakifanywa na kundi la MKO yangeweza kumrejesha tena madarakani. Hata hivyo kuchaguliwa Muhammad Rajai kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu kulimvunja moyo Bani Sadr ambaye aliamua kukimbilia Ufaransa akiwa amevaa nguo za kike.

Abul Hassan Bani Sadr na Mas'ud Rajavi 

Tarehe 29 Julai miaka 62 iliyopita Umoja wa Mataifa ulianzisha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). Lengo la kuanzishwa taasisi hiyo ya kimataifa, lilikuwa ni kusimamia shughuli zote za mitambo ya nyuklia na kuhakikisha kwamba miradi ya nyuklia duniani inatekelezwa kwa njia za amani na kutotumika kwa malengo ya kijeshi na utengenezaji wa silaha za mauaji ya halaiki.

Mkao Makuu ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki

Katika siku kama ya leo miaka 136 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 29 Julai 1883, alizaliwa Benito Mussolini mwanasiasa,  dikteta na mwasisi wa chama cha Kifashisti nchini Italia. Ufashisti ni utawala wa kidikteta uliojikita katika kuleta aidolojia ya kibaguzi na kiutaifa, kuwakandamiza wapinzani na kupotosha itikadi na fikra za wananchi. Mwaka 1922 Mussolini alinyakua wadhifa wa uwaziri mkuu wa Italia, na hivyo udikteta kuendelea kutawala nchini humo. Muda mfupi baadaye Mussolini alishirikiana na Adolph Hitler na kuandaa mazingira ya kuanza Vita vya Pili vya Dunia.

Benito Mussolini

Na miaka 718 iliyopita sawa na leo, alizaliwa mjini Quchan kaskazini mwa Iran, faqihi, mfasiri, mtaalamu wa itikadi na mwanafasihi wa Kiislamu Masud bin Omar Taftazani. Kwa kipindi kirefu cha umri wake Masud Taftazani alifanya safari katika miji ya Khorasan na Asia ya kati kwa lengo la kusoma.

 

Tags