Oct 10, 2019 04:22 UTC
  • Alkhamisi, 10 Oktoba, 2019

Leo ni Alkhamisi tarehe 11 Safar 1441 Hijria sawa na tarehe 10 Oktoba 2019

Miaka 288 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa huko katika mji wa Nice Ufaransa,  Henry Cavendish mwanafalsafa na tabibu wa Kiingereza. Cavendish alikuwa mwalimu wa masomo ya fikizikia na kemia. Henry Cavendish alikuwa mtu wa kwanza aliyethibitisha kuwa gesi ya hyadrogen ni nyepesi zaidi kuliko hewa ya kawaida. Cavendish aliaga dunia mwaka 1810.

Henry Cavendish

Tarehe 10 Oktoba miaka 138 iliyopita, kuliundwa muungano wa nchi tatu za Austria, Ujerumani na Italia. Kabla ya Italia kujiunga na muungano huo, awali kulikuwa na muungano wa mihimili miwili kati ya Austria na Ujerumani. Moja ya vipengee vya muungano huo kilikuwa na kusaidiana nchi wanachama pindi mmoja wao atakaposhambuliwa. Muungano huo ulikuwa ukiongezewa muda kila baada ya miaka mitano.

Miaka 107 iliyopita katika siku kama ya leo, mfumo wa Jamhuri nchini China ulichukua hatamu baada ya kuangushwa mfumo wa Kifalme. Katika kipindi cha kati ya mwaka 1907 na 1911 kulitokea uasi mara tano nchini China dhidi ya familia ya Kifalme ya Manchu. Uasi wote huo chimbuko lake kwa namna moja au nyingine lilikuwa ni fikra za kimapinduzi za Sun Yat-Sen mwanamapambano mashuhuri wa China. Hata hivyo uasi wa tano ambao ulianza tarehe 9 Oktoba mwaka 1911 ulipelekea kutokea ukandamizaji mkubwa, kutiwa mbaroni watu na mamia ya wengine kunyongwa hali ambayo ililipua ghadhabu na hasira za watu.

Kongresi ya Watu wa China

Na miaka 49 iliyopita katika siku kama ya leo, nchi ya Fiji ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza na siku kama hii husherehekewa nchini humo ikijulikana kama siku ya taifa. Fiji ilikuwa koloni rasmi la Uingereza tangu mwaka 1874 na Uingereza iliendelea kuukoloni muungano wa visiwa vya Fiji na ukoloni huo uliendelea kwa zaidi ya miaka 90. Mwaka 1965 katiba mpya ilianza kutekelezwa huko Fiji ambapo sheria zilibuniwa kwa ajili ya kupigania mamlaka ya kujitawala nchi hiyo.

Bendera ya Fiji

 

Tags