Serikali ya Saudi Arabia imewaruhusu Waislamu ambao hawajachanjwa dhidi ya virusi vya Corona, au ambao hawajakamilisha chanjo hiyo kufanya ibada ya Umra na kuingia Msikiti Mtakatifu wa Makka na Msikiti wa Mtume mjini Madina.
Katibu Mkuu wa harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah amesema inasikitisha kuona Saudi Arabia ikiwazuia Waislamu kutoka maeneo mengine ya dunia kutekeleza ibada ya Hija kwa mwaka wa pili mfululizo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe kwa Waislamu wote duniani kwa mnasaba wa siku hizi za Hija akisema kuwa kuendelea majonzi ya nyoyo za Waislamu wenye hamu kubwa ya kushiriki katika ugeni wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu ni mtihani wa muda na wa kupita.
Ibada tukufu ya Hija ilianza rasmi jana nchini Saudi Arabia chini ya usimamizi na sheria kali za kukabiliana na maambukizo ya virusi vya Corona huku idadi ya Mahujaji ikiwa chache mno.
Wizara ya Hija na Umra ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, ibada ya Hija mwaka huu itafanyika kwa kushirikisha raia na wageni wanaoishi nchini humo wasiozidi elfu 60.
Wizara ya Hija ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, watu waliopewa chanjo ya corona ndio watakaoruhusiwa kufanya ibada ya Umra katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kutekeleza ibada ya Swala katika Msikiti wa Makka.
Waziri wa Afya wa Saudi Arabia ametangaza kuwa, kupata chanjo ya virusi vya corona ni sharti muhimu kwa watu wote wanaoazimia kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
Serikali ya Saudi Arabia imewaruhusu mahujaji kutoka nje kuingia nchini humo kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Umra baada ya kufungwa mwezi Machi mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Serikali ya Saudi Arabia imetangaza rasmi kwamba wageni kutoka nchi za nje hawataruhuusiwa kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
Waziri wa Hija wa Saudi Arabia amewataka Waislamu kote duniani kuchelewesha maandalizi ya ibada ya mwaka huu ya Hija hadi pale hali ya mambo kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona duniani itakapobaika vyema.