-
UN, AU na EU zaahidi kushirikiana kwa ajili ya amani na maendeleo barani Afrika
Sep 23, 2025 02:57Viongozi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika AU na Umoja wa Ulaya EU, wametilia mkazo tena dhamira yao ya kuendeleza amani na maendeleo endelevu barani Afrika, kwa kuahidi ushirikiano wa kina zaidi ili kukomesha migogoro, kuimarisha mnepo na kukabiliana na changamoto za kimataifa kuanzia madeni hadi mabadiliko ya tabianchi.
-
Sababu za kuongezeka maradufu mauzo ya Iran barani Afrika
Sep 20, 2025 02:33Mauzo ya Iran barani Afrika yameongezeka maradufu.
-
Africa CDC: Kwa muda wa wiki moja, kesi za Ebola zimeongezeka zaidi ya maradufu mkoani Kasai, DRC
Sep 12, 2025 10:27Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Maradhi, (Africa CDC) kimetangaza kuwa, idadi ya watu wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa hatari wa Ebola katika jimbo la Kasai kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka zaidi ya maradufuu katika muda wa wiki moja tangu ulipothibitishwa mripuko mpya wa ugonjwa huo katika eneo hilo.
-
Mkutano wa pili wa hali ya hewa Afrika wazinduliwa Addis Ababa, Ethiopia
Sep 09, 2025 07:11Mkutano wa Pili wa Hali ya Hewa wa Afrika ulizinduliwa jana huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia huku viongozi wakitoa wito wa kuachana na utoaji matamshi pekee na kujikita katika uchukuaji hatua.
-
Afrika CDC: Mpox bado ni dharura ya kiafya barani Afrika
Sep 05, 2025 07:04Ugonjwa wa Mpox ambao umeenea katika nchi za Kiafrika na kuua mamia ya watu, bado ni dharura ya kiafya katika bara hilo. Taarifa hii imetolewa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC).
-
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Zambia ahukumiwa kifungo cha miaka 4 jela kwa ufisadi
Sep 04, 2025 13:14Mahakama ya Zambia leo Alhamisi imemhukumu Joseph Malanji aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kifungo cha miaka minne jela na kazi ngumu kwa kupatikana na hatia ya ufisadi.
-
AU yatiwa wasiwasi na makubaliano ya mataifa ya Afrika kupokea wahamiaji wa Marekani
Sep 02, 2025 06:26Baraza la haki la Umoja wa Afrika (AU) limeelezea wasiwasi wake kuhusu makubaliano ya Washington na nchi kadhaa za Afrika, ambayo yanaruhusu nchi hizo za Kiafrika kupokea wahamiaji waliofukuzwa Marekani.
-
14 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Namibia
Aug 31, 2025 07:24Wafanyakazi 11 wa Idara ya Huduma ya Marekebisho ya Namibia, afisa wa polisi na raia wawili wamepoteza maisha jana Jumamosi katika ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la kusini-kati nchini humo.
-
Botswana yatangaza dharura ya kiafya huku kukiwa na uhaba mkubwa wa dawa
Aug 26, 2025 15:01Botswana imetangaza dharura ya kiafya huku nchi hiyo ikikabiliwa na upungufu mkubwa wa dawa na vifaa tiba. Uhaba huo umesababisha hospitali na zahanati nchini humo kuhangaika kutibu magonjwa kuanzia shinikizo la damu, kisukari hadi saratani.
-
Wanahabari wa Afrika waunda Muungano wa Kupinga Mauaji ya Kimbari ya Israel Gaza
Aug 25, 2025 02:59Waandishi wa habari kutoka bara zima la Afrika wamezindua muungano uliopewa jina la 'African Journalists Against Genocide (AJAG)' wenye lengo la kupinga kile wanachoeleza kuwa ni mauaji ya kimbari ya Israel na uhalifu wa kivita dhidi ya watu wa Gaza, wakiwemo wanahabari wenzao.