-
Hofu yatanza juu ya uwezekano wa kuibuka mzozo mpya Ethiopia
Apr 21, 2026 10:25Chama kikuu cha siasa katika eneo la Tigray kaskaizni mwa Ethiopia kimetangaza kuwa kinachukua udhibiti wa serikali ya eneo hilo, na hivyo kubatilisha makubaliano ya amani na Serikali ya Shirikisho ya Ethiopia ambayo yalihitimisha moja ya migogoro mibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika karne hii.
-
Burundi, UNHCR kuwarejesha makwao wakimbizi wa Kongo
Apr 21, 2026 09:24Serikali ya Burundi, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), imetangaza mpango wa kuwarejesha makwao kwa hiari maelfu ya wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaoishi nchini humo.
-
Iran yailaani Israel kwa kukiuka mamlaka ya kitaifa ya Somalia
Apr 21, 2026 08:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hatua ya utawala wa kizayuni wa Israel ya kuteua mjumbe wa kidiplomasia huko Somaliland ni ishara wazi ya njama ya utawala huo ya kuvuruga amani na utulivu na kuchochea migawanyiko baina ya nchi za Kiislamu na za Kanda hiyo.
-
Rais wa Afrika ya Kati afichua sura mpya ya ukoloni
Mar 07, 2026 14:25Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema katika: "Diplomasia ya adhabu na vikwazo ni barakoa mpya ya ukoloni."
-
Waafrika 1,700 wadaiwa kushiriki katika vita vya Russia, Ukraine
Feb 26, 2026 01:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha amedai kwamba, zaidi ya Waafrika 1,700 wanapigana kwa niaba ya Russia katika vita vyake dhidi ya Ukraine, na kuongeza kwamba Moscow inatumia hadaa kuwasajili jeshini raia hao wa Kiafrika.
-
Waziri wa Ulinzi: Uhusiano na nchi za Afrika za kimapinduzi na zenye misimamo huru utastawishwa
Feb 23, 2026 23:01Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia kutekelezwa sera ya msingi ya kuendeleza na kustawisha uhusiano na nchi zenye misimamo huru na za kimapinduzi katika bara la Afrika Magharibi, hususan Burkina Faso.
-
Utumwa, ukoloni; Ghana yataka nchi za AU kuunga mkono Azimio la Algiers
Feb 16, 2026 06:44Rais wa Ghana ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kuunga mkono rasimu ya azimio lenye lengo la kutambua dhulma za kihistoria zilizosababishwa na biashara ya utumwa wa kuvuka Atlantiki.
-
Waziri Mkuu wa Ethiopia ahimiza kuwepo uhusiano wa heshima kati ya Afrika na Italia
Feb 15, 2026 04:26Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia amehimiza kuhusu ushirikiano mpya kati ya Afrika na Ulaya unaozingatia utu na ustawi wa pamoja. Waziri Mkuu wa Ethiopia ameeleza haya alipokuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Italia na Afrika mjini Addis Ababa mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Katibu Mkuu wa UN: Lazima Afrika iwe na sauti na iweze kunufaika na rasilimali zake
Feb 14, 2026 06:26Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito mkali wa kuhakikisha haki na mageuzi yanatekelezwa na kuimarishwa ushirikiano wa kimataifa, huku akiutaja Umoja wa Afrika AU, kama “kinara wa ushirikiano wa kimataifa katika dunia iliyogawanyika”.
-
Rais Xi Jinping wa China: Tutaziondolea ushuru nchi za Afrika ifikapo mwezi Mei
Feb 14, 2026 06:25Rais Xi Jinping wa China ametangaza kuwa, nchi yake itaziondolea ushuru nchi zingine za Afrika ifikapo mwezi Mei mwaka huu.