Iran yailaani Israel kwa kukiuka mamlaka ya kitaifa ya Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137872-iran_yailaani_israel_kwa_kukiuka_mamlaka_ya_kitaifa_ya_somalia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hatua ya utawala wa kizayuni wa Israel ya kuteua mjumbe wa kidiplomasia huko Somaliland ni ishara wazi ya njama ya utawala huo ya kuvuruga amani na utulivu na kuchochea migawanyiko baina ya nchi za Kiislamu na za Kanda hiyo.
(last modified 2026-04-21T08:20:33+00:00 )
Apr 21, 2026 08:03 UTC
  • Ismail Baqaei
    Ismail Baqaei

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema hatua ya utawala wa kizayuni wa Israel ya kuteua mjumbe wa kidiplomasia huko Somaliland ni ishara wazi ya njama ya utawala huo ya kuvuruga amani na utulivu na kuchochea migawanyiko baina ya nchi za Kiislamu na za Kanda hiyo.

Ismail Baqaei, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amesisitiza kuwa hatua hiyo ya upande mmoja ya utawala wa kizayuni inapingana wazi wazi na Hati ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa na inahesabiwa kuwa ukiukaji wa mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi ya nchi inayojitawala.

Aidha, amekumbusha wajibu wa Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Umoja wa Afrika na nchi zote kukabiliana na uvunjaji wa sheria, na sera za utawala haramu wa Israel za kutaka kujipanua na kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Katika siku za hivi karibuni, Umoja wa Afrika na zaidi ya nchi 10 za Kiislamu na Kiarabu zimeilaani hatua ya utawala wa kizayuni wa Israel ya kuteua balozi katika eneo lililotangaza kujitenga na Somalia la “Somaliland” lililoko kaskazini magharibi mwa Somalia.