Hofu yatanza juu ya uwezekano wa kuibuka mzozo mpya Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137884-hofu_yatanza_juu_ya_uwezekano_wa_kuibuka_mzozo_mpya_ethiopia
Chama kikuu cha siasa katika eneo la Tigray kaskaizni mwa Ethiopia kimetangaza kuwa kinachukua udhibiti wa serikali ya eneo hilo, na hivyo kubatilisha makubaliano ya amani na Serikali ya Shirikisho ya Ethiopia ambayo yalihitimisha moja ya migogoro mibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika karne hii.
(last modified 2026-04-21T10:29:54+00:00 )
Apr 21, 2026 10:25 UTC
  • Hofu yatanza juu ya uwezekano wa kuibuka mzozo mpya Ethiopia

Chama kikuu cha siasa katika eneo la Tigray kaskaizni mwa Ethiopia kimetangaza kuwa kinachukua udhibiti wa serikali ya eneo hilo, na hivyo kubatilisha makubaliano ya amani na Serikali ya Shirikisho ya Ethiopia ambayo yalihitimisha moja ya migogoro mibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika karne hii.

Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) imeeleza haya katika chapisho lale lililotumwa katika mtandao wa Facebook kikiituhumu Serikali ya Shirikisho ya Ethiopia kuwa imekiuka Mkataba wa Pretoria, uliohitimisha vita vya miaka miwili.

Taarifa ya harakati ya TPLF imeeleza kuwa, serikali ya Addis Ababa imechochea mzozo wa kivita ndani ya eneo la Tigray, imezuia fedha za kuwalipa watumishi wa serikali wa eneo hilo na kuongeza muda wa rais wa utawala wa mpito bila kushauriana na harakati hiyo.