-
"Akthari ya madini yanayohitajika na sekta ya nishati duniani yapo Afrika"
Feb 06, 2024 07:31Rais wa Afrika Kusini amesema aghalabu ya madini ya thamani yanayohitajika katika mageuzi makubwa kwenye sekta ya nishati duniani yanapatikana katika ardhi ya Afrika.
-
Papa adai Maaskofu wa Afrika wanapinga kubarikiwa 'mashoga' kwa sababu ya imani za kiutamaduni
Jan 30, 2024 23:13Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amesema, upinzani kutoka kwa maaskofu wa kikatoliki barani Afrika kwa agizo lake la kuwaruhusu makasisi kubariki watu wa jinsia moja wanaoishi kiunyumba, ni "kesi maalumu" inayochochewa na imani zao za kiutamaduni.
-
Katibu Mkuu wa UN: Afrika inapaswa kuwa na mwakilishi katika Baraza la Usalama
Jan 21, 2024 04:17Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelikosoa Baraza la Usalama la umoja huo kwa kutokuwa na mwakilishi wa kudumu kutoka Afrika. Guterres amehoji katika ukurasa wake wa X kwamba: "Je, tunawezaje kukubali kwamba Afrika haina hata mwanachama mmoja wa kudumu katika Baraza la Usalama?"
-
Baada ya Mauritius na Algeria, Cape Verde yawa nchi ya tatu barani Afrika kutokomeza Malaria
Jan 13, 2024 02:46Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitangaza Cabo Verde kuwa nchi isiyo na Malaria kwa kufanikiwa kuutokomeza ugonjwa huo na kuipatia cheti rasmi cha uthibitisho.
-
Ripoti: Israel inapanga kuwahamishia Afrika Wapalestina wa Gaza
Jan 04, 2024 23:02Vyombo vya habari vya Israel vimethibitisha ripoti zinazodai kuwa, utawala wa Kizayuni unafanya mazungumzo ya siri ili kuwahamisha kwa nguvu mamilioni ya wakazi wa Ukanda wa Gaza na kuwapeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na katika nchi nyingine za Afrika.
-
Kiongozi wa zamani wa upinzani Chad ateuliwa kuwa Waziri Mkuu
Jan 02, 2024 03:34Serikali ya mpito ya Chad imemteua Succes Masra, kiongozi wa zamani wa upinzani ambaye alirejea nchini humo hivi karibuni kutoka uhamishoni, kuwa Waziri Mkuu.
-
M’membe: Vikwazo vya Magharibi vimezikurubisha pamoja Russia, Afrika
Dec 25, 2023 07:12Rais wa Chama cha Kisoshalisti cha Zambia amesema nchi za Magharibi zinaziburuza nchi nyingine duniani kuingia vitani huku zikipora rasilimali zao.
-
Zaidi ya dola bilioni 1.8 kukusanywa ili kusaidia utengenezaji wa chanjo barani Afrika
Dec 08, 2023 22:58Taasisi ya Kimataifa ya Muungano wa Chanjo Gavi imetangaza maamuzi kadhaa iliyochukua ambayo yatasaidia nchi zenye kipato cha chini kukabiliana na athari za janga la COVID-19 na kuziwezesha kukabiliana na majanga ya kiafya katika siku zijazo. Maamuzi haya yamechukuliwa katika mkutano wa siku mbili chini ya uwenyeji wa serikali ya Ghana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Accra.
-
Iran: Afrika ina hamu ya kufufua utambulisho wake
Nov 30, 2023 00:23Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisiasa amesisitizia haja ya kuimarishwa uhusiano na ushirikiano wa Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika ikiwemo Senegal katika nyuga mbalimbali.
-
Makumi wauawa Sierra Leone, wafungwa 2,000 watoroka jela
Nov 28, 2023 02:36Makumi ya watu waliuawa huku wafungwa karibu 2,000 wakitoroka jela katika mashambulio ya Jumapili dhidi ya kambi ya jeshi, gereza na maeneo mengine nchini Sierra Leone.