-
Afrika Kusini yatangaza kukumbwa na maafa baada ya mafuriko kuathiri majimbo 7
Feb 14, 2023 08:41Afrika Kusini imetangaza maafa ya kitaifa baada ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni nchini humo kuuwa watu saba. Watu wengine wengi hawajulikani walipo hadi sasa. Haya yameelezwa na Kituo cha Kukabiliana na Majanga katika majimbo kadhaa nchini Afrika Kusini.
-
Afrika Kusini yatangaza hali ya maafa kufuatia kukatika umeme
Feb 10, 2023 03:26Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye amekabiliwa na lawama na ghadhabu za wananchi, jana alitangaza "hali ya maafa nchini humo kufautia kukosekana huduma ya umeme na kuahidi kumaliza shida ya upungufu wa nishati ambayo inatishia utulivu wa kiuchumi na kisiasa nchini humo.
-
Ziara ya kiduru ya Lavrov katika nchi za Afrika; jitihada za Russia za kuzidisha satwa yake barani Afrika
Jan 28, 2023 08:50Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Jumatatu tarehe 23 mwezi huu alianza safari ya kiduru kwa kuzitembelea nchi kadhaa za Kiafrika na hadi sasa amefanya safari huko Afrika Kusini, Eswatini, Angola na Eritrea.
-
Lavrov atetea maneva ya baharini na Afrika Kusini akiwa ziarani nchini humo
Jan 23, 2023 23:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kwamba Moscow haitaki kile alichokiita “chokochoko” zozote kuhusu mazoezi ya pamoja ya majeshi ya majini kati ya nchi hiyo, China na Afrika Kusini yaliyopangwa kufanyika mwezi ujao.
-
Afrika Kusini yasema BRICS inatafakari kutupilia mbali sarafu ya dola ya Marekani
Jan 18, 2023 07:27Nchi za Jumuiya ya BRICS ya mataifa yanayoibukia kiuchumi inataka kutupilia mbali sarafu ya dola ya Marekani na badala yake kuunda mfumo bora wa malipo ambao hautapendelea nchi tajiri.
-
Nyumba 200 zateketezwa kwa moto nchini Afrika Kusini
Jan 02, 2023 23:34Moto mkubwa uliotokea katika kitongoji duni nje kidogo ya mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini umeua mwanamke mmoja na kuharibu zaidi ya nyumba 200.
-
Afrika Kusini yapinga Israel kujiunga na Umoja wa Afrika
Dec 17, 2022 08:05Waziri wa Mambo ya Nje wa wa Afrika Kusini amesema kujiunga utawala wa Kizayuni wa Israel na Umoja wa Afrika ni sawa na tusi kwa moyo wa hati ya umoja huo.
-
Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini: Ramaphosa hatajiuzulu
Dec 04, 2022 03:32Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye yupo chini ya mashinikizo ya kutakiwa ajiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi inayomzunguka amesisitiza kuwa kiongozi huyo hatoachia ngazi.
-
Ramaphosa atakiwa kujiuzulu kwa tuhuma za ufisadi, mwenyewe amezikanusha
Dec 02, 2022 07:27Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini anakabiliwa na miito mbalimbali inayomtaka ajiuzulu baada ya uchunguzi wa Bunge kubaini kuwa huweda alikiuka sheria za kupambana na ufisadi kuhusiana na wizi wa mamilioni ya dola katika shamba lake la Phala Phala.
-
Maandamano yafanyika Afrika Kusini kulaani kuachiwa Mzungu katili
Dec 01, 2022 23:13Wananchi wa Afrika Kusini wamefanya maandamano kulalamikia hatua ya mahakama ya nchi hiyo kumuachia huru raia mbaguzi wa Poland aliyemuua mmoja wa viongozi waliokuwa wanapinga utawala wa zamani wa ubaguzi wa rangi (apartheid).