Afrika Kusini: Wafanyakazi wa sekta ya umma waandamana, wadai nyongeza ya mishahara
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i95086-afrika_kusini_wafanyakazi_wa_sekta_ya_umma_waandamana_wadai_nyongeza_ya_mishahara
Muungano wa wafanyakazi wa skta ya umma nchini Afrika Kusini wamendelea kuandamana nje ya hospitali kadhaa nchini humo. Maandamano hayo ambayo yamewajumuisha wanachama wa vyama vya wafanyakazi katika masuala ya afya na elimu, yameingia katika wiki yake ya pili sasa huku vyombo vya usalama vikiimarisha usalama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 14, 2023 04:14 UTC
  • Afrika Kusini: Wafanyakazi wa sekta ya umma waandamana, wadai nyongeza ya mishahara

Muungano wa wafanyakazi wa skta ya umma nchini Afrika Kusini wamendelea kuandamana nje ya hospitali kadhaa nchini humo. Maandamano hayo ambayo yamewajumuisha wanachama wa vyama vya wafanyakazi katika masuala ya afya na elimu, yameingia katika wiki yake ya pili sasa huku vyombo vya usalama vikiimarisha usalama.

Muungano wa Elimu ya Taifa, Afya na Wafanyakazi Washirika wa Afrika Kusini unataka nyongeza ya mishahara ya asilimia 10 huku serikali ikisema kuwa itatoa nyongeza ya asilimia 4.7 tu. Wafanya maandamano wameapa kuendelea na maandamano yao hadi pale matakwa yao yatakapopatiwa ufumbuzi.  

Jeshi la Afrika Kusini limetangaza kuwa, wafanyakazi wa sekta ya afya na matibabu walitumwa katika hospitali kadhaa za umma nchini humo ili kupunguza athari za mgomo ambao serikali inasema umesababisha vifo vya watu kadhaa hadi sasa.

Joe Phaahla Waziri wa Afya wa Afrika Kusini amesema kuwa wagonjwa wasiopungua wanne wamega dunia na kwamba vifo vyao huenda vimechangiwa na mgomo wa wafanyakazi unaoendelea. 

Wiki iliyopita, wafanyakazi wa sekta ya afya waliogoma Afrika Kusini waliweka vizuizi katika hospitali mbalimbali na hivyo kuzuia wagonjwa kuingia kwa ajili ya kupatiwa matibabu.