Pars Today
Zaidi ya wahajiri 250 wanaaminika kuwa wamezama baharini baada ya mitumbwi miwili waliyokuwa wakisafiria kugunduliwa na boti ya uokozi katika pwani ya Libya.
Kikosi cha ulinzi katika pwani ya Libya kimearifu kuwa wahajiri zaidi ya 120 wameokolewa majini karibu na bandari ya Tripoli kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Vikosi vya doria katika pwani ya Italia vimetangaza kuwa vimewaokoa wahajiri 1,300 katika bahari ya Mediterania.
Wahajiri na wakimbizi wapatao 219 wamezama katika Bahari ya Mediterranea katika wiki mbili za kwanza za mwaka 2017 hii ikiwa ni mara mbili zaidi ya kipindi sawa na hiki mwaka jana.
Makumi ya wahajiri wanahofiwa kupoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kwenda bara Ulaya kuzama katika Bahari ya Mediterranea.
Shirika la Kimataifa la Uhajiri (IOM) limesema wakimbizi na wahajiri wapatao 5,000 wamepoteza maisha mwaka huu wa 2016 wakijaribu kuingia barani Ulaya kupitia Bahari ya Mediterranea.
Maafisa husika wa Morocco wameeleza kuwa wahajiri wanne wameaga dunia baada ya kuzama boti yao iliyokuwa imebeba makumi ya wahajiri katika maji ya bahari ya Mediterania kati ya Morocco na Uhispania.
Wahajiri zaidi ya 200 wamenusurika kufa maji baada ya kuokolewa katika bahari ya Mediterania.
Zaidi ya wahajiri 240 wamefariki dunia au kutoweka katika bahari ya Mediterenia huku wengine 580 wakiokolewa kutoka kwenye boti zilizofurika wahajiri hao haramu.
Umoja wa Mataifa umesema wahajiri 239 wali0kuwa wakielekea barani Ulaya wamepoteza maisha baada ya boti zao kuzama katika pwani ya Libya.