-
Indhari kuhusu ubaguzi katika utoaji chanjo ya COVID-19 duniani
Mar 16, 2021 02:37Ingawa kugunduliwa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 au corona ni jambo ambalo liliibua matumaini duniani kote, lakini ugavi usio wa kiudilifu wala usawa wa chanjo hiyo ni jambo ambalo limewakasirisha wengi na hata kuibua kelele katika baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya. Kuhusiana na nukta hiyo Kansela Sebastian Kurz wa Austira amesema hakuna uadilifu katika usambazwaji chanjo ya COVID-19 barani Ulaya.
-
Nchi 6 za Ulaya zisimamisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca
Mar 12, 2021 02:41Denmark imekuwa nchi ya sita ya Ulaya kusimamisha matumizi ya chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 ya AstraZeneca kutokana na madhara yake kwa damu za watu waliopigwa chanjo hiyo.
-
Kenya yazindua kampeni ya kitaifa ya chanjo ya kupambana na corona
Mar 05, 2021 12:24Kenya hii leo imezindua kampeni ya kitaifa ya chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, huku Patrick Amoth, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Afya akiwa Mkenya wa kwanza kuchanjwa katika ardhi ya nchi hiyo.
-
DRC: Chanjo milioni 1.7 za Covid 19 za AstraZeneca zawasili nchini
Mar 03, 2021 08:10Zaidi ya dozi milioni moja na laki saba za chanjo ya Covid-19 zilizotengenezwa na Kampuni ya AstraZeneca jana Jumanne zilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa N'djili huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia mpango wa COVAX.
-
Iran yapokea dozi robo milioni za chanjo ya Corona kutoka China
Feb 28, 2021 13:21Shehena ya kwanza ya dozi za chanjo ya kubaliana na ugonjwa wa Covid-19 kutoka China imewasili hapa nchini Iran leo Jumapili.
-
Wahanga nusu milioni wa virusi vya corona nchini Marekani, sababu na taathira zake
Feb 24, 2021 02:41Baada ya kupita mwaka mmoja sasa tangu kulipotokea mlipukowa ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani na kufeli kwa serikali ya nchi hiyo katika kukabiliana na janga hilo, sasa idadi ya wahanga wa corona imepindukia watu nusu milioni kwa kadiri kwamba, Rais Joe Biden amemuru bendera za nchi hiyo zipepee nusu mlingoti.
-
Mawaziri watatu wakumbwa na ugonjwa wa corona nchini Misri
Feb 22, 2021 14:03Mawaziri watatu wa Misri yaani waziri wa biashara na viwanda, waziri wa mahakama na waziri wa fedha wamekumbwa na ugonjwa wa COVID-19.
-
Mkuu mpya wa WTO ataka usawa katika ugavi wa chanjo za Corona
Feb 16, 2021 07:59Mkuu mpya wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) ametahadharisha dhidi ya 'utaifa' katika ugawaji wa chanjo za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 na kusisitiza kuwa, janga la Corona linaweza kudumaza ukuaji wa uchumi wa nchi zote duniani, maskini na hata tajiri.
-
Watu zaidi ya 95,000 wamepoteza maisha kutokana na corona Afrika
Feb 09, 2021 10:55Watu waliopoteza maisha barani Afrika kutokana na ugonjwa wa corona au COVID-19 sasa wamepindukia 95,000 huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi katika wiki zijazo.
-
Shehena ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 ya Russia yawasili Iran
Feb 04, 2021 14:15Shehena ya kwanza ya chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona ya Sputnik V ya Russia imewasili hapa nchini Iran leo Alkhamisi.