-
Mfululizo wa vipindi vya vinavyokosoa mienendo ya magenge potofu ya kigaidi na ukufurishaji/ sehemu ya 24 pamoja na sauti
Mar 09, 2017 10:16Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni tena katika mfululizo wa vipindi hivi vinavyokosoa kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu na suna za Bwana Mtume (saw) makundi ya ukufurishaji yanayotekeleza jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wengine hii ikiwa ni sehemu ya 24 ya mfululizo huo.
-
Daesh laua zaidi ya watu 30 katika hospitali ya kijeshi Afghanistan
Mar 08, 2017 12:33Wanamgambo waliojizatiti kwa silaha nzito wameua zaidi ya watu 30 na kuwajeruhi wengine wapatao 50 katika shambulio walilofanya dhidi ya hospitali kubwa zaidi ya kijeshi ya Sardar Daud Khan iliyopo katikati mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
-
Mafanikio makubwa huko Iraq; kukimbia Daesh kutoka Mosul hadi Raqqa
Mar 08, 2017 04:06Ushindi vilioupata vikosi vya jeshi la Iraq katika mji wa Mosul kukiwemo kudhibiti majengo muhimu ya serikali umewapelekea makamanda wa kundi la kigaidi la Daesh kuwataka magaidi waukimbie mji wa Mosul na kuelekea Raqqa nchini Syria.
-
Waziri Mkuu wa Iraq: Daesh hawana njia isipokuwa kujisalimisha au kuuliwa
Mar 07, 2017 23:49Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh hawana njia nyingine isipokuwa kujisalimisha au kuuawa.
-
Jengo la redio ya genge la Daesh, Mosul ladhibitiwa na jeshi la Iraq
Mar 04, 2017 12:34Habari kutoka mkoa wa Nainawa (Nineveh) nchini Iraq zinaarifu kwamba jeshi la nchi hiyo limedhibiti jengo la redio ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh kwa jina la al-Bayan.
-
Daesh latumia gesi ya sumu kujaribu kulizuia jeshi la Iraq kuyakomboa maeneo yaliyosalia Mosul
Mar 03, 2017 00:49Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limetumia silaha zenye gesi ya sumu katika kulizuia jeshi la Iraq kusonga mbele katika maeneo yaliyosalia.
-
Hatimaye kinara wa Daesh akiri kushindwa nchini Iraq, awataka wafuasi wake kukimbilia milimani
Mar 01, 2017 01:10Kinara wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) Abubakar al-Baghdadi ametoa hotuba ya mwisho akikiri kushindwa kundi hilo nchini Iraq na amewataka wafuafi wake kukimbilia maeneo ya milimani kwa usalama wao au kujiripua.
-
Syria: Tunashirikiana kwa karibu na Iraq katika kupambana na genge la Daesh
Feb 25, 2017 10:56Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesisitizia uepo wa ushirikiano baina ya nchi yake na serikali ya Iraq katika kupambana na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS).
-
Russia yasema itapiga kura ya veto dhidi ya muswada wa Baraza la Usalama kuhusu Syria
Feb 25, 2017 03:47Russia imetangaza kuwa, itatumia kura ya veto kupinga vikwazo vya aina yoyote ile vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Syria kwa madai kwamba nchi hiyo imetumia silaha za kemikali.
-
HRW: Wanawake ni wahanga wa vitendo vya ubakaji vya kundi la Daesh nchini Iraq
Feb 20, 2017 12:30Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, wanawake nchini Iraq ni wahanga wa vitendo vya ubakaji vinavyofanywa na kundi la kigaidi la Daesh.