Mar 08, 2017 03:19 UTC
  • Waziri Mkuu wa Iraq: Daesh hawana njia isipokuwa kujisalimisha au kuuliwa

Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh hawana njia nyingine isipokuwa kujisalimisha au kuuawa.

Haider al-Abadi amewaambia makamanda wa jeshi al Iraq katika mji uliokombolewa wa Mosul kwamba kundi la kigaidi la Daesh liko katika siku zake za mwisho nchini Iraq. 

Waziri Mkuu wa Iraq amewataka wakazi wa mji wa Mosul kushirikiana na jeshi na askari usalama wa Iraq kwa ajili ya kuliangamzia kikamilifu kundi hilo la kigaidi na kurejesha amani katika eneo hilo.

Haider al-Abadi jana alikwenda katika mji wa Mosul kukagua maendeleo ya jeshi la nchi hiyo ambalo linaendela kukomboa majengo na idara za serikali kutoka mikononi mwa mabaki ya kundi la kigaidi la Daesh. 

Askari wa kikosi maalumu cha jeshi la Iraq, Mosul

Kikosi maalumu cha jeshi la Iraq jana Jumanne kilifanikiwa kukomboa majengo ya serikali katika mji huo wa Mosul ambao ulikuwa makao makuu ya kundi la kiwahabi la Daesh nchini iraq.

Ripoti zinasema wapiganaji wa kundi hilo sasa wanakimbia huko na kule na kwamba baadhi ya makawanda wao walionusurika kifo wanaelekea katika mji wa Raqqa nchini Syria.  

Tags