-
Javad Zarif ajibu ujumbe wa Trump aliyeitaka Iran kuketi kwenye meza ya mazungumzo Marekani
Jun 05, 2020 22:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu pendekezo la Rais Donald Trump wa Marekani kwa Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo mapya akisema kuwa, Iran au pande nyingine za mapatano ya nyuklia ya JCPOA, hazijawahi kuondokwa kwenye meza ya mazungumzo.
-
Malalamiko ya UN dhidi ya ubaguzi wa rangi wa kitaasisi nchini Marekani
Jun 05, 2020 01:27Ubaguzi wa rangi na kizazi na ukandamizaji uliochupa mipaka dhidi ya watu wasio wazungu hasa wenye asili ya Afrika huko Marekani una historia ndefu na ulianza tangu ilipoasisiwa nchi hiyo karne tatu zilizopita. Ubaguzi huo daima umekuwa ni sifa inayochukiza ya jamii ya Marekani. Licha ya Wamarekani wenye asili ya Afrika kuendesha mapambano makali ya kupigania haki zao, lakini hadi leo hii wanaendelea kuwa wahanga wa ubaguzi, ukatili na ukandamizaji usio na kifani.
-
Obama ataka mageuzi Marekani, Pelosi ajiunga na waandamanaji dhidi ya ubaguzi wa rangi
Jun 04, 2020 08:16Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kufanyika marekebisho katika mfumo wa jeshi la polisi la nchi hiyo na kusisitiza kuwa, waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi wanapaswa kuwanyima utulivu wanaoshikilia madaraka.
-
Wasiwasi wa Pentagon na hata Republican kwa hatua ya Trump ya kutumia wanajeshi kukandamiza waandamanaji Marekani
Jun 04, 2020 08:11Maandamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea mfano wake huko Marekani yamemtia kiwewe na kumuweka kwenye hali ngumu rais wa nchi hiyo mwenye majigambo na majivuno mengi, Donald Trump na kumfanya atoe amri ya kutumiwa jeshi, suala ambalo limelalamikiwa na Wizara ya Ulinzi, lakini hata wanachama wenzake ndani ya chama cha Republican nao hawakubaliani na uamuzi wake wa kutumia nguvu za kijeshi kukandamiza waandamanaji.
-
Hata 'Mbwa Kichaa' akosoa mienendo ya Trump; zaidi ya 10,000 wakamatwa katika maandamano Marekani
Jun 04, 2020 03:25Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis maarufu kwa jina la "Mbwa Kichaa" ametangaza kuwaunga mkono wananchi wa Marekani wanaondamana kulaani ubaguzi wa rangi na mienendo ya kikatili ya polisi ya Marekani hususan dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika.
-
Tishio la Trump la kutuma jeshi la taifa katika majimbo ya Marekani kukabiliana na wapinzani wa ubaguzi
Jun 03, 2020 08:02Malalamiko na maandamano makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika miji na majimbo ya Marekani dhidi ya mauaji ya kutisha yaliyofanywa na polisi dhidi ya raia mweusi wa nchi hiyo, George Floyd huko katika jimbo la Minnesota yamezusha machafuko makubwa na kumtia kiwewe rais wa nchi hiyo, Donald Trump na serikali yake.
-
Wasiwasi wa Ulaya kuhusu kushamiri mrengo wa fikra za kibaguzi nchini Marekani
Jun 02, 2020 23:22Fikra za kuchupa mipaka za mrengo wa kulia zimeshamiri sana nchini Marekani katika kipindi cha uongozi wa Donald Trump kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
-
Trump asisitiza kuwakandamiza waandamanaji wanaolalamikia ubaguzi wa rangi nchini Marekani
Jun 02, 2020 01:54Ubaguzi wa rangi na matumizi ya mabavu dhidi ya wale wanaotajwa kuwa watu wa rangi nchini Marekani na hasa weusi, ni jambo lenye historia ndefu nchini humo. Licha ya mapambano ya muda mrefu ya weusi kwa ajili ya kutetea haki zao, lakini wangali ni wahanga wakubwa wa ubaguzi na matumizi ya mabavu na hasa kutoka kwa polisi ya nchi hiyo.
-
Trump awatisha waandamanaji wanaolalamikia ukatili Polisi Marekani dhidi ya Wamarekani Weusi
May 30, 2020 03:44Ukatili usio na kikomo wa Jeshi la Polisi nchini Marekani dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika au Wamarekani weusi ambao unafanyika katika fremu ya sera jumla za ubaguzi wa rangi dhidi ya kaumu hiyo umeibua malalamiko makubwa katika siku za hivi karibuni nchini humo. Malalamiko hayo yameibuka baada ya Mmarekani mweusi kuuawa kinyama siku chache zilizopita mikononi mwa afisa wa polisi mzungu.
-
Baada ya vitisho, hatimaye Trump akata uhusiano na WHO
May 30, 2020 03:40Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kukata uhusiano na Shirika la Afya Duniani WHO, akidai kuwa taasisi hiyo ya kimataifa ni kikaragosi cha China.