"Trump anaongoza magaidi waliovaa tai huko White House"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61452-trump_anaongoza_magaidi_waliovaa_tai_huko_white_house
Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesisitiza kuwa, wananchi waliostaarabika wa Iran wanamtambua vyema mkuu wa magaidi waliovaa tai katika Ikulu ya Marekani, White House.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 06, 2020 11:40 UTC

Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesisitiza kuwa, wananchi waliostaarabika wa Iran wanamtambua vyema mkuu wa magaidi waliovaa tai katika Ikulu ya Marekani, White House.

Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo leo kujibu mapendekezo ya rais wa Marekani, Donald Trump ya kufanya mazungumzo na Tehran na kusema, haiwezekani kwa upande mmoja Trump aongoze ugaidi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad na kumuua kidhulma shujaa wa dunia wa kupambana na ugaidi na upande wa pili ajifanye kuwa hana matatizo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na yuko tayari kufanya nayo mazungumzo.

Hossein Amir-Abdollahian, Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) 

Ikumbukwe kuwa Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Jeshi la Quds la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH tarehe 3 Januari mwaka huu aliuliwa kigaidi kwa amri ya rais wa Marekani, Donald Trump karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq akiwa mgeni rasmi wa serikali ya nchi hiyo tena uraiani si katika uwanja wa vita.

Hata hivyo, Trump anajifanya kusahau jinai na ugaidi wote huo, na jana Ijumaa aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, Wairan wasisubiri hadi kumalizika uchaguzi ujao Marekani kwa ajili ya kufikia makubaliano makubwa.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyeuliwa kigaidi na kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani huko Iraq kwa amri ya Donald Trump

 

Trump amejigamba pia kuwa yeye ndiye atakayeshinda katika uchaguzi wa rais wa Marekani uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu na kuitaka Iran ifanye mazungumzo naye.

Kabla ya hapo, Dk Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikuwa amejibu ujumbe huo wa Twitter wa Trump kwa kusema, Ni Marekani ndiyo iliyojitoa kwenye makubaliano ya JCPOA na kwenye meza ya mazungumzo, si upande mwingine wowote. Aidha amemwambia Trump kwamba: Washauri wako (ambao wengi wao umeshawafukuza) wamecheza kamari ya kijinga na kipuuzi, sasa hivi kila kitu kinategemea wewe mwenyewe, ni lini utakirekebisha.