Trump apongeza polisi ya Marekani, apuuza kilio cha waandamanji kuhusu ubaguzi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i61553-trump_apongeza_polisi_ya_marekani_apuuza_kilio_cha_waandamanji_kuhusu_ubaguzi
Rais Donald Trump wa Marekani amelipongeza jeshi la polisi nchini humo huku akipuuzilia mbali kilio cha waandamanaji ambao wanasema kuna ubaguzi mkubwa katika jeshi hilo.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Jun 11, 2020 22:36 UTC
  • Trump apongeza polisi ya Marekani, apuuza kilio cha waandamanji kuhusu ubaguzi

Rais Donald Trump wa Marekani amelipongeza jeshi la polisi nchini humo huku akipuuzilia mbali kilio cha waandamanaji ambao wanasema kuna ubaguzi mkubwa katika jeshi hilo.

Trump ameyasema hayo Alhamisi huku maandamano yakiendelea nchini Marekani baada ya polisi mzungu mbaguzi kumuua kinyama Mmarekani mwenye asili ya Afrika.

Mnamo Mei 25, afisa wa polisi katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesta nchini Marekani alimbinya shingo kwa kutumia goti kwa dakika 9 hivi George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye asili ya Afrika hadi akakata roho.

Mauaji hayo ya kinyama yaliibua maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa Marekani kupinga ubaguzi wa rangi huku miito ikitolewa ya kulifanyia marekebisho jeshi la polisi nchini humo.

Polisi mzungu alivyomuua George Floyd

Katika hotuba yake jana, Trump amedai kuwa ni maafisa wachache wabaya katika jeshi la polisi.  Hadi sasa Trump amekataa kuzungumza wazi wazi kuhusu ukatili wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi huki akidai kuwa maudhui hiyo si muhimu.

Hayo yanajiri wakati ambao sanamu zinazoashiria ubaguzi zimeangushwa, kuharibiwa ama kuondolewa na waandamanaji katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sanamu la Christopher Columbus mjini Boston na sanamu ya Edward Colston aliyekuwa mfanyabiashara wa watumwa, katika karne ya 17.