-
Abiy Ahmed: Waasi wa OLA wameua raia wengine kwa umati Oromia
Jul 06, 2022 01:48Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amelituhumu kundi la waasi linalojiita Jeshi la Ukombozi wa Oromo (OLA) kuwa limefanya mauaji mapya ya halaiki katika eneo la Oromia, magharibi mwa nchi.
-
AU yataka Sudan, Ethiopia ziache makabiliano ya kijeshi mpakani
Jun 30, 2022 03:42Kamisheni ya Umoja wa Afrika imetoa mwito kwa nchi za Sudan na Ethiopia kujizuia na kutochukua hatua yoyote inayoweza kushadidisha mivutano ya kijeshi katika eneo la al-Fashaqa, lililoko katika mpaka wa pamoja wa nchi mbili hizo jirani.
-
Khartoum yaituhumu Addis Ababa kuwanyonga wafungwa wa Sudan na kuonyesha miili yao
Jun 27, 2022 22:21Jeshi la Sudan limelitumu jeshi la Ethiopia kuwa limewanyonga wanajeshi 7 na raia mmoja wa Sudan waliokuwa wafungwa nchini humo, jambo ambalo limekanushwa na maafisa rasmi wa Ethiopia, wakieleza kuwa Addis Ababa itatoa tamko rasmi la kujibu madai hayo ya Sudan.
-
Mvutano baina ya Ethiopia na Sudan: Jeshi la Ethiopia latuhumiwa kuwaua Wasudan wanane
Jun 27, 2022 03:26Sudan imesema, jeshi la Ethiopia limeua raia wanane wa nchi hiyo.
-
Bachelet ataka uchunguzi huru wa mauaji ya halaiki nchini Ethiopia
Jun 24, 2022 09:56Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa sambamba na kulaani mauaji ya halaiki ya hivi karibuni ya raia hususan wanawake na watoto wadogo magharibi mwa Ethiopia, ameitaka serikali ya Addis Ababa kufanya uchunguzi huru, wa kina, wa haraka na usioegemea upande wowote.
-
WFP: Maisha ya Waethiopia milioni 20 yako hatarini kutokana na vita, ukame na uhaba wa chakula
Jun 23, 2022 22:44Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limetahadharisha kuwa, baa la njaa linazidi kutishia maisha ya Waethiopia milioni 20 ambao wanakabiliwa na vita kaskazini mwa nchi hiyo, ukame katika eneo la kusini na kupungua kwa msaada wa chakula na lishe kuanzia mwezi ujao.
-
Iran yalaani shambulio lililoua mamia ya watu nchini Ethiopia
Jun 21, 2022 03:24Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio lililopelekea kuuawa mamia ya watu katika eneo la Oromia nchini Ethiopia, na kueleza kuwa Tehran imesikitishwa mno na mauaji hayo ya halaiki.
-
Manusura wa mauaji ya halaiki ya Oromia wasimulia: Watu waliuawa kama kuku
Jun 20, 2022 22:15Mwangwi wa mauaji ya halaiki yanayodaiwa kufanywa na waasi dhidi ya raia ambao wengi wao ni kutoka kabila la Amhara huko Ethiopia unaendelea kusikika huku baadhi ya manusura wakieleza jinsi mauaji hayo ya kutisha yalivyofanyika.
-
Ethiopia yabuni kamati ya kuzungumza na wapiganaji wa Tigray
Jun 14, 2022 22:12Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema serikali ya federali ya nchi hiyo imeunda kamati ya kufanya mazungumzo na vikosi vya Harakati ya Ukombizi wa Watu wa Tigray (TPLF).
-
UN yataka Kenya, Somalia na Ethiopia zisaidiwe kukabili ukame
May 21, 2022 08:00Umoja wa Mataifa umetoa mwito wa dharura wa kupatikana fedha ili kusaidia mataifa ya Pembe ya Afrika ambayo kwa miezi yameshuhudia hali ya ukame inayotishia kuwa mbaya zaidi.