Raia wengi wameuawa Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i85640-raia_wengi_wameuawa_ethiopia
Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Ethiopia imesema raia wasiopungua 749 wameuawa katika mikoa ya Afar na Amhara katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika mapigano ambayo yamejiri kati ya vikosi vya jeshi la serikali na waasi wa Tigray People's Liberation Front TPLF.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 09, 2022 02:38 UTC
  • Raia wengi wameuawa Ethiopia

Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Ethiopia imesema raia wasiopungua 749 wameuawa katika mikoa ya Afar na Amhara katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika mapigano ambayo yamejiri kati ya vikosi vya jeshi la serikali na waasi wa Tigray People's Liberation Front TPLF.

Ikitangaza habari hiyo hapo jana Ijumaa, Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Ethiopia imesema idadi hiyo ya raia waliuawa katika kipindi cha kati ya mwezi Juni mwaka uliopita wa 2021 na mwezi huu wa Julai mwaka huu.

Mapigano  hayo yaliyojiri kwa muda wa miezi 20 yalijiri katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi na kuenea hadi maeneo ya Amhara kaskazini magharibi na Afar magharibi mwa nchi hiyo.

Daniel Bickley, mkuu wa Kamisheni ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia, amesema kuwa idadi hiyo ya wahanga sio idadi ya mwisho inayotokana na mapigano hayo na kwamba uchunguzi zaidi kuhusu kadhia hiyo bado unaendelea.

Wahanga wa mapigano ya Tigray

Viongozi wa kieneo wa Ethiopia wametangaza karibuni hivi kwamba zaidi ya watu 200 wameuawa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wanaofungamana na kabila la Amhara katika eneo la Oromia.

Mzozo wa Tigray ambao unahesabiwa kuwa wa kikabila ulianza tangu kuingia madarakani Abiy Ahmad, Waziri Mkuu wa Ethiopia mwaka 2018, jambo ambalo limechochea ghasia na machafuko katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo katika mpaka nchi jirani za Eritrea na Sudan. Kundi la magaidi wa as-Shabaab pia linajishughulisha na vitendo vya ugaidi nchini humo.