Pars Today
Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa imekomboa miji mikubwa katika eneo la Amhara kutoka kwa "magenge la wanamgambo waasi", baada ya siku kadhaa za vita kati ya jeshi la serikali kuu na wanamgambo wa eneo hilo.
Afisa wa ngazi ya juu wa Ethiopia amewatuhumu wanamgambo katika eneo la Amhara kuwa wanataka kupindua serikali za jimbo na ya shirikisho kufuatia mapigano ya siku kadhaa mtawalia ambayo yamepelekea mamlaka za uongozi kutangaza hali ya hatari.
Ethiopia, ambayo ni miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika imeomba kujiunga na jumuiya ya BRICS ya chumi zinazoinukia. Haya yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.
Ethiopia inajiandaa kuanzisha awamu ya nne ya kujaza maji katika hifadhi ya bwawa lake kubwa katika Blue Nile. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo licha ya upinzani wa jirani yake Misri.
Mamlaka za Ethiopia zimewarejesha nyumbani raia 80 wa Uganda ambao walitapeliwa fedha zao kwa ahadi kwamba watapelekwa kukutana na Yesu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Serikali ya Ethiopia imepinga ripoti iliyotolewa na Shirika la Haki za Binadamu la (HRW) iliyodai kuwa kampeni ya maangamizi ya kizazi imefanyika huko Tgray Magharibi licha ya kutiwa saini makubaliano ya amani mwezi Novemba mwaka jana.
Watu wawili wameuawa wakati askari polisi walipowashambulia Waislamu walioandamana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kupinga kubomolewa misikiti yao zaidi ya 19 katika eneo la kandokando ya mji huo.
Waasi katika jimbo la Oromia nchini Ethiopia wameituhumu serikali kuu ya nchi hiyo kuwa imefanya mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi yao baada ya mazungumzo ya amani kati ya pande mbili kumalizika bila kufikia mapatano.
Askari usalama wa Ethiopia wametangaza kuwa wamewakamata watu 47 kufuatia mauaji ya afisa wa chama tawala nchini humo.
Shirika la Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) linachunguza wizi wa misaada ya chakula ulioripotiwa katika oparesheni za kibinadamu huko Ethiopia.