-
Meli kubwa ya mafuta yalipuka baada ya kukanyaga mabomu ya majini kwenye njia haramu kusini mwa Hormuz
Sep 15, 2026 04:15Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetangaza kuwa meli kubwa ya kubeba mafuta ghafi (supertanker) iliyojaribu kupita bila idhini katika eneo lililopigwa marufuku kusini mwa Lango Bahari la Hormuz imelipuka baada ya kukanyaga mabomu ya kutega majini, huku chombo hicho chote kikiwa kimeteketea na kufunikwa na miali mikubwa ya moto.
-
Iran: mkutano wa Oman ni hatua muhimu kuelekea utulivu na usalama wa kikanda
Sep 13, 2026 07:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mkutano uliopangwa kufanyika nchini Oman Jumatatu ya kesho utakuwa hatua muhimu kuelekea kuhakikisha utulivu na usalama katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Iran: Mlango Bahari wa Hormuz unabaki kwenye udhibiti wetu kamili; dunia iilaumu US kwa kupanda bei ya mafuta
Sep 13, 2026 07:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesisitiza kuwa Mlango wa Bahari wa Hormuz unasalia kuwa chini ya udhibiti kamili wa Iran, akisema Marekani ndiye wa kulaumiwa kwa kuvurugika usalama wa baharini wa eneo hilo na inapasa ilaumiwe pia kwa kupanda bei ya mafuta duniani.
-
Meja Jenerali Rezaei: Iran itaainisha 'eneo jipya la marufuku' nje ya Mlango-Bahari wa Hormuz
Sep 07, 2026 03:37Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC) amesema, eneo jipya la marufuku nje ya Mlango-Bahari wa Hormuz litatangazwa katika siku zijazo, akionya kwamba chombo chochote kitakachoingia katika eneo hilo bila mashauriano na Tehran kitawekwa kwenye orodha ya vikwazo vya Iran.
-
PGSA: Iran itazuilia na kutwaa meli zinazokiuka sheria za Lango-Bahari la Hormuz
Aug 24, 2026 06:15Mamlaka ya Lango-Bahari la Ghuba ya Uajemi (PGSA), ambayo ni chombo cha udhibiti cha Iran cha Lango-Bahari la Hormuz, imetangaza kwamba meli zinazokiuka itifaki za Iran za njia hiyo ya majini ya kimkakati zitakabiliwa na vikwazo kwenye njia za baadaye, ikiwa ni pamoja na faini, kuzuiliwa, au kutwaliwa.
-
Mkuu wa Usalama: Iran itaendelea kufunga Hormuz hadi Marekani itimize majukumu yake
Aug 23, 2026 14:24Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itafubaza mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani ikiwa ni pamoja na kuzichukulia hatua nchi ambazo zinashiriki katika “vita vya kiuchumi” vya Marekani dhidi ya Iran.
-
Mkuu wa Idara ya Mahakama amwambia Trump: Iran ndiyo mmiliki na mtawala wa Lango la Hormuz
Aug 16, 2026 05:56Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Gholam-Hossein Mohseni-Eje’i, amezitaja kauli za hivi karibuni za Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu umiliki wa Lango Bahari la Hormuz kuwa ni "upuuzi," akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ndiyo mmiliki na mtawala halisi wa lango hilo.
-
Rezaei: Mlango-Bahari wa Hormuz utafunguliwa ikiwa tu US itayakubali masharti ya Iran
Aug 12, 2026 12:33Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema, kufunguliwa tena kikamilifu Mlango-Bahari wa Hormuz katika Ghuba ya Uajemi, ambao umewekewa vizuizi vya uvukaji na Iran tangu mwanzoni mwa mwezi Machi kutokana na uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel kutafanyika pale tu Marekani itakapoyakubali masharti ya Iran.
-
Araqchi: Mazungumzo na Oman kuhusu Lango-Bahari la Hormuz yako katika hatua za mwisho
Aug 09, 2026 11:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema leo kwamba mazungumzo na Oman kuhusu Lango Bahari la Hormuz yako katika hatua za mwisho na kuongeza: "Bila shaka, hii haina maana kwamba Lango la Hormuz litafunguliwa. Ufunguzi wa Lango la Hormuz unategemea masharti mengine."
-
Zolqadr: Lango-Bahari la Hormuz litaendelea kufungwa hadi pale Marekani itakapobadilisha tabia yake
Aug 09, 2026 09:55Afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa nchi hiyo haitalegeza vikwazo vya usafirishaji kupitia Lango Bahari la Hormuz hadi pale Marekani itakapobadilisha mwenendo wake mbele ya Tehran.