-
Badala ya kulaani jinai za Israel; Imarati ndio kwanza yatoa vitisho kwa Wapalestina
May 16, 2021 11:57Huku jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel zikizidi kuwa kubwa dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza, chombo kimoja cha habari cha utawala wa Kizayuni kimefichua kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umeonesha uungaji mkono wake kwa jinai hizo za Wazayuni kupitia kutoa vitisho vipya dhidi ya Wapalestina.
-
Imarati yatakiwa kuangalia upya uhusiano, mapatano yake na Israel
May 08, 2021 12:20Muungano wa Muqawama Dhidi ya Kuanzishwa Uhusiano na Israel wa Umoja wa Falme za Kiarabu umeitaka serikali ya Imarati, wafanyabiashara na shakhsia huru wa nchi hiyo ya Kiarabu kuangalia upya mapatano ya ushirikiano yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya UAE na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mwanafalsafa mtajika wa Ujerumani akataa tuzo ya kifahari ya UAE
May 04, 2021 01:33Msomi na mwanafalsafa mashuhuri wa Ujerumani amekataa kupokea tuzo ya kifahari ya uandishi wa vitabu kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kutokana na kile kinachoonekana ni kutoafiki mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo ya Kiarabu na historia yake ya ukiukaji wa haki za binadamu.
-
Mamluki wa Saudia na Imarati wapigana wao kwa wao kusini mwa Yemen
Apr 12, 2021 11:24Mamluki wa kundi linalojiita Baraza la Mpito la Kusini lenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na wale wa serikali iliyojiuzulu ya Yemen wenye mfungamano na Saudi Arabia kwa mara nyingine tena wamepigana wao kwa wao huko kusini mwa Yemen.
-
Wanaharakati wa nchi za Kiarabu waanzisha kampeni ya kuisusia UAE kwa kuuza bidhaa za Israel
Apr 09, 2021 02:38Wanaharakati wa mitandao ya kijamii katika nchi za Kiarabu wameanzisha kampeni ya kuususia Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati kwa kuuza bidhaa za Israel kwa kutumia chapa za biashara za Jordan na za eneo la Ufukwe wa Magharibi katika masoko ya nchi hiyo na kwa kuzisafirisha pia katika nchi zingine za Ghuba ya Uajemi.
-
Ukosoaji kufuatia kuongezeka hatua za Imarati za kujipenyeza kiintelijinsia na kisiasa huko Iraq
Mar 31, 2021 10:42Katika masiku ya karibuni suala la kujipenyeza Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko Iraq kwa mara nyingine tena limezungumziwa pakubwa. Shakhsia na vyombo vya habari vya Iraq vimetangaza kuwa Imarati imezidisha satwa yake ya kiintelijinsia na kisiasa nchini humo.
-
Imarati yakosoa hatua ya Netanyahu kutumia vibaya safari ya Abu Dhabi kwa malengo ya uchaguzi
Mar 22, 2021 02:30Kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) amekosoa hatua ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala haramu wa Israel, ya kutumia vibaya mapatano na nchi za Kiarabu kwa ajili ya manufaa yake binafsi na kuongeza kuwa utawala wa Abu Dhabi ulitia saini mapatano hayo kwa lengo la kufikiwa amani na sio masuala ya uchaguzi.
-
Ansarullah: Hii ndiyo sababu iliyotufanya tuache kuishambulia kijeshi Imarati
Mar 19, 2021 08:04Kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Asarullah ya Yemen amefichua kuwa, barua ya kiongozi wa harakati hiyo, Sayyid Abdul Malik al Houthi kwa Umoja wa Falme za Kiarabu iliyoipelekea Abu Dhabi ikomeshe mashambulio yake nchini Yemen, ndiyo sababu iliyoifanya Ansarullah isimamishe mashambulizi yake ya kulipiza kisasi dhidi ya Imarati.
-
Serikali ya Somalia yaikosoa Imarati kwa kuwaunga mkono wapinzani wa Kisomali
Feb 21, 2021 15:16Serikali ya Somalia imeikosoa Imarati kutokana na kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Mogadishu.
-
Kuendelea mapigano kati ya Imarati na Saudia huko Yemen
Feb 18, 2021 09:34Mamluki wenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko kusini mwa Yemen wamevishambulia vikosi vya serikali iliyojiuzulu ya Yemen ya Abdrabbuh Mansur Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia wakati vilipokuwa vikielekea katika mkoa wa Maarib mashariki mwa Yemen.