Ansarullah: Hii ndiyo sababu iliyotufanya tuache kuishambulia kijeshi Imarati
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i68058-ansarullah_hii_ndiyo_sababu_iliyotufanya_tuache_kuishambulia_kijeshi_imarati
Kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Asarullah ya Yemen amefichua kuwa, barua ya kiongozi wa harakati hiyo, Sayyid Abdul Malik al Houthi kwa Umoja wa Falme za Kiarabu iliyoipelekea Abu Dhabi ikomeshe mashambulio yake nchini Yemen, ndiyo sababu iliyoifanya Ansarullah isimamishe mashambulizi yake ya kulipiza kisasi dhidi ya Imarati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 19, 2021 04:34 UTC
  • Ansarullah: Hii ndiyo sababu iliyotufanya tuache kuishambulia kijeshi Imarati

Kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Asarullah ya Yemen amefichua kuwa, barua ya kiongozi wa harakati hiyo, Sayyid Abdul Malik al Houthi kwa Umoja wa Falme za Kiarabu iliyoipelekea Abu Dhabi ikomeshe mashambulio yake nchini Yemen, ndiyo sababu iliyoifanya Ansarullah isimamishe mashambulizi yake ya kulipiza kisasi dhidi ya Imarati.

Muhammad Ali al Houthi, mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema hayo katika mtandao wa Twitter na kuongeza kuwa, baada ya Sayyid Abdul Malik al Houthi kuwaandikia barua viongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, nchi hiyo ilijitoa katika muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na ilikomesha mashambulio yake dhidi ya Yemen ndio maana Ansarullah nayo iliamua kukomesha mashambulizi yake dhidi ya Imarati. Katika upande mwingine, mashambulizi ya Ansarullah na jeshi la Yemen dhidi ya maeneo tofauti ya nchi vamizi ya Saudia yanaendelea.

Nembo ya harakati ya Kiislamu ya Ansarullah ya Yemen

 

Habari za karibuni kabisa ni mashambulizi yaliyofanywa na majeshi ya Yemen dhidi ya uwanja wa ndege wa Abha wa kusini magharibi mwa Saudia kwa kutumia ndege zisizo na rubani yaani drone. Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen alisema jana usiku katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, droni za Yemen zimefanya opresheni nyingine ya mafanikio katika uwanja wa ndege wa Abha wa nchini Saudi Arabia. Amefafanua zaidi kwa kuksema, katika mashambulizi hayo, ndege hizo za Yemen zimeshambulia sehemu ya kijeshi kwa kutumia droni aina ya Qasef K2 na operesheni hiyo imefanyika kwa mafanikio makubwa.

Tarehe 26 mwezi huu wa Machi, vita vya kivamizi vilivyoanzishwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi ya Kiarabu na Kiislamu ya Yemen vitaingia katika mwaka wake wa 7. Hadi hivi sasa zaidi ya watu 17,000 wameshauawa na makumi ya maelfu ya wengine wameshajeruhiwa na karibu Wayemen milioni 4 wamekuwa wakimbizi kutokana na uvamizi huo.