-
Vyama 28 vya siasa India kuungana dhidi ya Modi katika uchaguzi wa Mei 2024
Sep 02, 2023 07:33Vyama 28 vya upinzani nchini India vimeamua kushiriki kwa pamoja katika uchaguzi mkuu wa 2024 dhidi ya Waziri Mkuu Narendra Modi lengo likiwa ni kuzuia ushindi wa tatu mfululizo wa chama tawala cha Hindu Bharatiya Janata (BJP).
-
Hasira zatanda India baada ya mwalimu kuwataka watoto wamchape vibao mwanafunzi Muislamu
Aug 27, 2023 13:32Wimbi la hasira limeibuka nchini India baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii vidio inayomuonyesha mwalimu wa skuli moja katika jimbo la Uttar Pradesh akimdhalilisha mwanafunzi Muislamu darasani kwa kuwataka wanafunzi wenzake wamchape vibao na kutaka pia afukuzwe skulini hapo kwa sababu ya dini yake.
-
Wahindu wenye chuki na Uislamu wamuua Imamu na kuuchoma moto msikiti katika mji wa Gurugram, India
Aug 01, 2023 13:25Naibu Imamu wa Sala ya jamaa ameuawa baada ya kundi la Wahindu wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia kuufyatulia risasi na kuuchoma moto msikiti katika kitongoji cha mji mkuu wa India, New Delhi, saa chache baada ya ghasia mbaya za kijamii zilizozuka katika wilaya jirani.
-
Kupanuka zaidi mpasuko wa kidini nchini India
Jun 16, 2023 02:28Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni wa Kituo cha Utafiti wa Jamii Zinazoendelea (CSDS) huko New Delhi unaonyesha kuwa, sera za Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, zimezidisha mgawanyiko wa kidini nchini humo.
-
Chama cha Modi chang'olewa Karnataka, jimbo la India lililopiga marufuku Hijabu
May 14, 2023 11:27Chama cha upinzani cha Congress nchini India kimeshinda katika uchaguzi wa jimbo muhimu la Karnataka kusini mwa nchi hiyo na kuking'oa chama tawala cha Waziri Mkuu Narendra Modi, BJP mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa kitaifa.
-
Jibu na hatua za serikali ya India dhidi ya uasi uliozuka katika majimbo manane ya nchi hiyo
May 09, 2023 01:23Uasi katika jimbo la Manipur umeilazimisha serikali ya India kutuma vikosi vya uchukuaji hatua za haraka na kuweka marufuku ya kutotoka nje katika miji minane tofauti ya nchi hiyo.
-
Shamkhani asisitiza kuanzishwa utaratibu wa matumizi ya Riyali na Rupia
May 02, 2023 01:33Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametilia mkazo kuanzishwa utaratibu wa kutumia sarafu ya Riyali na Rupia katika mabadilishano ya kibiashara na kiuchumi kati ya Iran na India.
-
Licha ya India kukanusha, OIC: Waislamu walilengwa kichuki katika tamasha la Wahindu
Apr 05, 2023 11:41Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imesema, kushambuliwa Waislamu wakati wa tamasha la Wahindu la Ram Navami ni 'dhihirisho la wazi la kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu' nchini India.
-
Wahindu wenye msimamo mkali washambulia shule ya Kiislamu na kuchoma nakala za Qur'ani na maelfu ya vitabu
Apr 04, 2023 13:30Wanaharakati kwenye majukwaa ya mawasiliano ya kijamiii ya India wamechapisha picha zinazoonyesha shule ya Kiislamu ikiteketea kwa moto katika jimbo la Bihar, baada ya kushambuliwa na Wahindu wenye msimamo mkali siku ya Ijumaa, na kusababisha uharibifu mkubwa.
-
Serikali ya India yabomoa msikiti mwingine kwa kisingizio cha ujenzi wa barabara
Jan 17, 2023 07:28Serikali ya India imebomoa msikiti mwingine katika jimbo la Uttar Pradesh kwa kisingizio cha ujenzi wa barabara.