-
Sisitizo la viongozi wakuu wa Iran na Saudia la kuimarisha uhusiano baina ya nchi zao
Jul 19, 2024 05:26Mohammed bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na Massoud Pezeshkian, rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wamezungumza kwa simu na kutilia mkazo umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya Tehran na Riyadh.
-
Iran yakosoa sera za kindumakuwili za nchi za Magharibi kuhusiana na jinai za Israel
Jul 19, 2024 00:22Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Iran amekosoa madai yaliyotolewa dhidi ya Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na misimamo ya kindumakuwili kuhusiana na maripota maalumu wa jumuiya hiyo ya kimataifa.
-
Kanusho la Iran kwa madai ya uwongo ya Marekani ya kuhusika katika jaribio la kumuua Trump
Jul 18, 2024 07:10Baada ya tukio la kupigwa risasi Donald Trump, rais wa zamani na mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2024, baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani kwa mara nyingine vikiendeleza propaganda za chuki dhidi ya Iran (Iranphobia) vilidai kuweko mkono wa Iran katika tukio hilo.
-
Mrithi wa Ufalme wa Saudia ampongeza Rais mteule wa Iran
Jul 17, 2024 10:16Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad Bin Salman amemnyooshea mkono wa pongezi Masoud Pezeshkian, Rais Mteule wa Iran kwa kuibuka mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Bagheri Kani na Rais wa Baraza Kuu la UN wajadili mauaji ya Gaza
Jul 16, 2024 04:14Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuna udharura wa kuchukuliwa hatua za kivitendo ili kukomesha jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
China: Tuko tayari kushirikiana na serikali ijayo ya Iran
Jul 16, 2024 03:48Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema China inathamini uhusiano wake na Iran na iko tayari kushirikiana na serikali mpya ya Jamhuri ya Kiislamu ili kuendeleza ushirikiano wa kimkakati na wa kina kati ya pande mbili.
-
Iran katika maombolezo ya Tasua, yaitaka dunia ikabiliane na jinai za Israel
Jul 15, 2024 09:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran sanjari na kutoa mkono wa pole kwa Waislamu kote duniani ambao hii leo wapo katika maombelezo ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein AS, ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kivitendo za kusimamisha jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Iran ya Kiislamu yaghariki kwenye Tasua ya Imam Hussein AS
Jul 15, 2024 07:21Waislamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maeneo mengine ya dunia leo tarehe 9 Mfunguo Nne Muharram wameshiriki katika vikao, marasimu, majlisi na shughuli mbali mbali za maombolezo ya Tasua ya Imam Hussein AS, mjukuu wa Mtume wetu Muhammad SAW.
-
Kan’ani alaani madai ya Argentina ya kuwahusisha raia wa Iran katika mlipuko wa "Amia"
Jul 14, 2024 03:55Nasser Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, amelaani matamshi yasiyo na ushahidi ya Waziri wa Sheria wa Argentina na vile vile taarifa iliyotolewa na Ofisi wa Rais wa nchi hiyo ikiwatuhumu raia wa Iran kuwa walihusika katika mlipuko wa jengo la "Amia".
-
Iran: Israel haijali mstari wowote mwekundu wa maadili
Jul 14, 2024 03:36Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali jinai mpya iliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika eneo la Al-Mawasi huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya wakimbizi wa Kipalestina na kujeruhi mamia ya wengine.