-
Ukwamishaji mpya wa Marekani dhidi ya juhudi za Iran za kupambana na virusi vya corona
Jan 14, 2021 23:05Baada ya kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA hapo mnamo Mei 2018, na katika fremu ya kile kinachotajwa kuwa 'mashinikizo ya juu kabisa', Marekani imekuwa ikitekeleza vikwazo vikali zaidi katika historia yake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wala haijawahi kulegeza vikwazo hivyo vya kinyama hata katika kipindi hiki kigumu cha kuenea duniani virusi hatari vya corona.
-
Rouhani: Ongezeko la wawekezaji wa kigeni Iran ni ishara ya kufeli vikwazo vya Marekani
Jan 14, 2021 09:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ongezeko la asilimia 56 ya wawekezaji wa kigeni katika maeneo ya biashara huru nchini Iran ni ishara ya kufeli sera za Marekani za ugaidi wa kiuchumi na mashinikizo ya juu kabisa.
-
Marekani yaliwekea vikwazo shirika la Iran linalounda chanjo ya corona
Jan 14, 2021 09:36Marekani imekithirisha uhasama wake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuliwekea vikwazo shirika la Iran ambalo liko katika mstari wa mbele kuunda chanjo ya corona au COVID-19.
-
Russia yapuuzilia mbali bwabwaja mpya za Marekani dhidi ya Iran
Jan 13, 2021 23:09Russia imekosoa vikali madai ya kipropaganda ya Marekani ya kujaribu kulifungamanisha kundi la kigaidi la al-Qaeda na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pasi na kutoa ushahidi wowote.
-
Iran yailaani Marekani kwa kuiweka Cuba katika orodha ya 'waungaji mkono ugaidi'
Jan 13, 2021 04:42Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya Marekani kuiweka Cuba katika orodha ya nchi ambazo eti zinaunga mkono ugaidi. Iran aidha imesema inafungamana na Cuba katika mapamano yake dhidi ya madola ya kibeberu duniani.
-
Meli kubwa zaidi ya kivita iliyoundwa Iran yazinduliwa rasmi
Jan 13, 2021 04:38Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo limepokea meli yake kubwa zaidi ya kivita ambayo imeundwa nchini Iran. Meli hiyo kubwa ya kivita ambayo imeundwa kikamlifu na wataalamu wa Iran ina uwezo wa kusheheni helikopta kadhaa kwa ajili ya oparehseni muhimu za baharini.
-
Zarif: Kurejea Marekani JCPOA bila vikwazo kuondolewa si kwa maslahi ya Iran
Jan 13, 2021 01:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kurejea Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA bila Iran kuondolewa vikwazo ni kwa maslahi ya Marekani ni wala si kwa maslahi ya Tehran.
-
Waziri wa Ulinzi: Maadui wameshindwa kupigisha magoti Iran
Jan 13, 2021 01:12Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Amiri Hatami amesisitiza kuwa, maadui walidhani wangeipigisha magoti Iran lakini wameshindwa kabisa kutokana na Wairani kusimama kidete dhidi yao na sasa ni Rais Trump wa Markeani na waitifaki wake ndio wanaochukiwa zaidi na watu duniani na watatupwa katika dampo la taka za historia.
-
Jumatano, 13 Januari, 2021
Jan 12, 2021 23:31Leo ni Jumatano tarehe 29 Jamadil Awwal 1442 Hijria sawa na Januari 13 mwaka 2021.
-
Russia yajibu madai ya Pompeo dhidi ya Iran, yasema Iran ni muathirika wa silaha za kemikali
Jan 12, 2021 01:44Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Mashirika ya Kimataifa mjini Vienna, Mikhail Ulyanov amekanusha madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo kuwa eti Iran imetumia silaha za kemikali na kusema kuwa, Iran yenyewe ni muathiriak wa silaha hizo.