Mej. Salami: Taifa la Iran limepata ushindi katika vita vya kiuchumi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i67878-mej._salami_taifa_la_iran_limepata_ushindi_katika_vita_vya_kiuchumi
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa katika vita vya kiuchumi adui ameshindwa na taifa la Iran limepata ushindi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 14, 2021 07:41 UTC
  • Mej. Salami: Taifa la Iran limepata ushindi katika vita vya kiuchumi

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa katika vita vya kiuchumi adui ameshindwa na taifa la Iran limepata ushindi.

Meja Jenerali Hussein Salami,  Kamanda Mkuu wa IRGC ameyasema hayo Jumapili katika Kongamano la Nnne la Wahadhiri wa Taaluma ya Malezi katika Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iran, Basij. 

Meja Jenerali Salami ameongeza kuwa, adui ameshindwa na kupata pigo katika vita vya kiuchumi dhidi ya Iran.

Kamanda Mkuu wa IRGC ameongeza kuwa, taifa la Iran limekuwa na subira na halikukariri sauti ya adui wala halikumzingatia.

Kombora la Emad la Iran

Hali kadhalika Kamanda Mkuu wa IRGC amesisitiza kuwa, leo Iran ina uwezo mkubwa na wa kisasa kabisa. Ameongeza kuwa, Iran ina silaha na zana za kivita sawa na alizonazo adui.

Aidha Meja Jenerali Salami amesema adui anajidhihirisha kama mwenye nguvu lakini ukweli ni kuwa si chochote si lolote.