-
Kukiri mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani malengo halisi ya Washington dhidi ya Iran
Oct 18, 2020 23:00Tarehe 8 Mei 2018 Marekani chini ya utawala wa Donald Trump, ilijitoa kwenye mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA na kuiwekea Iran vikwazo vikubwa zaidi ambavyo havijawahi kutokea. Ijapokuwa awali serikali ya Trump ilidai kuwa inataka mapatano ya nyuklia ya JCPOA yaangaliwe upya ndio maana imejitoa kwenye makubaliano hayo, lakini hivi sasa inatangaza waziwazi lengo lake hasa la kujitoa kwenye mapatano hayo.
-
Zaidi ya wagonjwa wapya 4,000 wa corona wagunduliwa nchini Iran
Oct 17, 2020 08:16Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ametangaza habari ya kugunduliwa zaidi ya wagonjwa 4,000 wapya wa ugonjwa wa COVID-19 humu nchini na kufarikia dunia wagonjwa 253 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
-
Sisistizo la Russia la kushirikiana kijeshi na Iran baada ya kuondolewa vikwazo vya silaha
Oct 16, 2020 23:12Kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa vikwazo vya silaha vya Iran vinamalizika tarehe 18 mwezi huu wa Oktoba 2020 baada ya kumalizika muda wa miaka mitano wa vikwazo hivyo. Russia ikiwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama na moja kati ya nchi wanachama wa kundi la 4+1 imesisitiza kwamba itashirikiana kijeshi na Iran baada ya kumalizika vikwazo licha ya Marekani kufanya juhudi za kuongeza muda wa vikwazo hivyo.
-
Wanasayansi wa Iran wako imara kukabiliana na ubeberu wa Marekani
Oct 15, 2020 23:09Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran imetangaza kuwa, wanasayansi na wasomi wa Iran wako imara katika kukabiliana na ubeberu na uistikbari wa Marekani kwenye nishati ya nyuklia.
-
Iran yakosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa ubabe wa Marekani
Oct 15, 2020 04:21Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema uchukuaji hatua za upande mmoja wa Marekani ndilo tishio kuu kwa haki za binadamu duniani, huku akikosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa ubabe huo wa Washington.
-
Zarif: Uwepo wa vikosi ajinabi Mashariki ya Kati unashadidisha matatizo
Oct 15, 2020 00:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa uwepo wa wanajeshi ajinabi katika eneo la Mashariki ya Kati ni tete na unashadidisha matatizo mbalimbali. Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan.
-
Zaidi ya wagonjwa 4,800 wapya wa corona wagunduliwa Iran
Oct 14, 2020 09:11Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ametangaza kuwa, zaidi ya wagonjwa wapya elfu nne na mia nane (4,800) wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini katika kipindi cha saa 24 zlizopita.
-
Iran yachukua uwenyekiti wa Kundi la 24
Oct 14, 2020 04:15Gavana wa Benki Kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kundi la 24 (G24) katika kikao cha mawaziri wa fedha na magavana wa benki wa nchi wanachama kilichofanyika kwa njia ya intaneti.
-
Ndoto za alinacha za Trump za kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Oct 13, 2020 22:53Rais Donald Trump wa Marekani akiwa na lengo la kujijengea nafasi nzuri wakati huu wa kukaribia uchaguzi nchini humo, anahitajia kutoa madai ya kufanikiwa katika sera za kigeni za nchi hiyo hasa kuhusiana na Iran.
-
Namaki: Iran inapambana na vikwazo na corona kwa wakati mmoja
Oct 13, 2020 08:08Waziri wa Afya wa Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapambana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na virusi vya corona kwa wakati mmoja."