Iran na nchi kadhaa duniani zasimamisha safari za ndege za Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65315-iran_na_nchi_kadhaa_duniani_zasimamisha_safari_za_ndege_za_uingereza
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingine kadhaa duniani zimesimamisha kwa muda safari za ndege za kwenda na kutoka Uingereza baada ya kuripotiwa aina mpya ya msambao wa virusi vya corona mjini London na kusini mashariki mwa UK.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 21, 2020 04:49 UTC
  • Iran na nchi kadhaa duniani zasimamisha safari za ndege za Uingereza

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingine kadhaa duniani zimesimamisha kwa muda safari za ndege za kwenda na kutoka Uingereza baada ya kuripotiwa aina mpya ya msambao wa virusi vya corona mjini London na kusini mashariki mwa UK.

Shahram Adamnejad, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Ustawi wa Miji wa Iran amesema Tehran kwa kufuata miongozi ya wataalamu wa afya hapa nchini, imeamua kusimamisha kwa muda wa wiki mbili safari za ndege baina ya nchi mbili hizi, kutokana na kusambaa kwa kasi aina hiyo mpya ya virusi vya corona.

Kadhalika nchi kadhaa za Ulaya zikiwemo Ubelgiji, Uholanzi, Austria na Italia zimechukua hatua kama hiyo ya Iran. Aidha Ujerumani imeripotiwa kutafakari kufuata mkumbo huo wa kusimamisha kwa muda safari za anga baina yake na Uingereza.

Nchi nyingine zilizopiga marufuku ndege za Uingereza kutua katika ardhi zao kwa muda kutokana na msambao huo mpya wa corona ni Canada, Saudi Arabia, Uswisi, Sweden na Uturuki.

Ndege za shirika la British Airways la Uingereza

Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza ameeleza kuwa, aina hiyo ya spishi ya maambukizi ya corona inaenea kwa asilimia 70 kwa haraka zaidi ilikinganishwa na ile ya kabla yake.

Pamoja na hayo, hakuna ushahidi unaothibitisha kwamba, spishi hiyo mpya ya kirusi cha corona ni hatari zaidi  au chanjo ya corona itakuwa na athari ndogo kwa spishi hiyo.