Russia: Ushirikiano wetu na Iran katika masuala ya nishati ni muhimu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65366-russia_ushirikiano_wetu_na_iran_katika_masuala_ya_nishati_ni_muhimu
Mkuu wa Kituo cha Usalama wa Nishati cha Russia amegusia safari ya Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow na kusema kwamba, kustawishwa ushirikiano wa pande hizi mbili katika sekta za mafuta, gesi na vinu mbalimbali ni jambo muhimu sana. Amesema, mustakbali wa ushirikiano huo ni mzuri na uko wazi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 24, 2020 00:01 UTC
  • Russia: Ushirikiano wetu na Iran katika masuala ya nishati ni muhimu

Mkuu wa Kituo cha Usalama wa Nishati cha Russia amegusia safari ya Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow na kusema kwamba, kustawishwa ushirikiano wa pande hizi mbili katika sekta za mafuta, gesi na vinu mbalimbali ni jambo muhimu sana. Amesema, mustakbali wa ushirikiano huo ni mzuri na uko wazi.

Anton Khlopkov amesema hayo katika mahojiano na shirika la habari la IRNA na kuongeza kuwa, ushirkiano katika sekta za nishati kati ya Moscow na Tehran una umuhimu mkubwa kiasi kwamba Rais Vladimir Putin wa Russia anatambua kwamba ushirikiano kwenye sekta hiyo ni katika vipaumbele vikubwa vya uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amesema, serikali ya Russia inalipa umuhimu mkubwa suala la kushirikiana na Iran katika nyuga zote lakini hasa sekta za mafuta na gesi.

Waziri wa Mafuta wa Iran,  Bijan Namdar Zangeneh

 

Afisa huyo wa Russia ameongeza kuwa, ziara ya Bijan Namdar Zangeneh, Waziri wa Mafuta wa Iran mjini Moscow akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Tehran, ina umuhimu mkubwa hasa kwa kuzingatia hali iliyopo hivi sasa na hususan uratibu wa pamoja wa nchi hizi mbili katika kuhakikisha soko la mafuta duniani haliyumbi na vile vile kwa kuzingatia kuwa Iran na Russia ni madola makubwa duniani yanayozalisha gesi kwa wingi.

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo, Khlopkov amesema, Iran ni mwanachama muhimu wa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani OPEC na Russia nayo kwa upoande wake imetoa ushirikiano mkubwa kwa jumuiya hiyo katika miaka ya hivi karibuni. Amesema ni kwa sababu hiyo ndio maana mazungumzo ya Tehran na Mascow kuhusu hali ya soko la mafuta duniani na ushirikiano na wazalishaji wengine wa mafuta ulimwenguni, yana umuhimu mkubwa.