-
Swala ya Idul Adh'ha yafanyika katika maeneo mbalimbali ya Iran ya Kiislamu kwa kufuata protokali za afya
Jul 31, 2020 03:46Swala ya Idul Adh'ha imefanyika leo asubuhi katika miji mbalimbali ya Iran ya Kiislamu kwa kufuata protokali za afya.
-
Zaidi ya wagonjwa 259,000 wa Covid-19 nchini Iran wamepata afueni
Jul 29, 2020 10:31Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, wagonjwa wengine wapya wapatao elfu mbili wa maradhi ya Covid-19 wamegunduliwa nchini, huku idadi ya waliopata afueni ya ugonjwa huo ikipindukia 259,000.
-
Rouhani: Adui hajaweza kuizuia Iran kuuza bidhaa nje ya nchi
Jul 29, 2020 03:15Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema adui hajaweza kuizuia Iran kuuza bidhaa zake nje ya nchi.
-
Jumanne tarehe 28 Julai mwaka 2020
Jul 27, 2020 23:23Leo ni Jumanne tarehe 7 Dhulhija 1441 Hijria sawa na Julai 28 mwaka 2020.
-
Uhusiano wenye mlingano na madola yote ya Eurasia, Asia Mashariki na Kusini, kipaumbele katika sera za kigeni za Iran
Jul 26, 2020 06:16Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma ya kulinda na kuendeleza mlingano wa uhusiano na urafiki na madola yote makubwa ya Eurasia, Asia Mashariki na Kusini.
-
Balozi wa Syria Tehran: Uchokozi wa Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran ni ugaidi
Jul 25, 2020 22:11Balozi wa Syria mjini Tehran amesema, uchokozi wa ndege za kivita za Marekani dhidi ya ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria ni nembo na dhihirisho la ugaidi wa Marekani dhidi ya raia wakiwemo wanawake na watoto.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran yakemea vikali hatua ya ndege zakivita za Marekani ya kuhatarisha usalama wa ndege ya abiria ya Iran
Jul 24, 2020 09:19Msemaji wa Wizara Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekemea vikali hatua ya ndege mbili za kijeshi za Marekani ya kutishia usalama wa ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria na kusema: Habari zaidi kuhusu tukio hilo zinafanyiwa uchunguzi na hatua za dharura za kisiasa na kisheria zitachukuliwa baada ya kukamilika uchunguzi huo.
-
Ufunguo wa kutatua mgogoro wa Syria ni kulindwa mamlaka ya kujitawala na wananchi kuwa na nafasi katika utawala
Jul 24, 2020 08:54Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kulindwa mamlaka ya kujitawala, mipaka na uhuru wa kisiasa Syria ni mambo ya dharura na pia wanajeshi wote wa kigeni walioko Syria wanapaswa kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo mara moja.
-
Mousavi: Moto wa karibuni nchini Iran hauhusiani na hujuma za kimtandao
Jul 23, 2020 02:54Akijibu madai kuhjusu uharibifu na hujuma za kimtandao dhidi ya Iran, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, moto uliotokea hivi karibuni hapa nchini hausiani kivyovyote na hujuma za kimtandao.
-
Rouhani: Uhuru wa kujitawala na usalama wa Iran na Iraq vinafungamana
Jul 21, 2020 22:00Rais Hassan Rouhani wa Iran na Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi wamesema uhusiano wa Tehran an Baghdad unavuka mipaka ya nchi mbili hizi jirani, na kusisitiza kuwa: Uhuru wa kujitawala na usalama wa Iran na Iraq vina mfungamano mkubwa.