Borell akiri udharura wa Iran kunufaika na mkataba wa JCPOA
Licha ya kuwa Umoja wa Ulaya na Troika ya Ulaya ambayo inajumuisha nchi za Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zilikuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama JCPOA, lakini baada ya Marekani kujitoa katika mapatano hayo, pande hizo zimekuwa na utendaji mbaya usioweza kutetewa kutokana na kuwa zimeshindwa kuyalinda na pia kutotekeleza ahadi zao, na hasa kuhusu kutofanikisha mfumo wa mabadilishano ya kifedha na kibiashara unaojulikana kama Instex.
Akiashiria udharura wa Iran kunufaika na mapatano ya JCPOA katika Bunge la Ulaya siku ya Jumatano, Joseph Borrell, Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya alidai kwamba nchi za Ulaya zitafanya kila linalowezekana ili kuongezeka kiwango cha mabadilishano ya kibiashara na Iran. Alisema mapatano hayo ya Iran hayahusiana tu na suala la nyuklia bali yanahusu pia masuala ya biashara na uchumi. Borell amedai kuwa pamoja na kuwa ni vigumu kwa Iran kustafidi na mapatano hayo kutokana na vikwazo vya upande mmoja ilivyowekewa na Marekani lakini Umoja wa Ulaya utafanyika kila linalowezekana ili kutekeleza ahadi zake katika fremu ya mapatano hayo. Mkuu huyo wa siasa za kigeni za Umoja wa Ulaya ameashiria hatua ya Marekani ya kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran na kusema kuwa Marekani haina haki yoyote ya kutumia mchakato wa vikwazo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikia lengo hilo.
Kukiri Borell kuhusu Iran kunyimwa haki ya kunufaika na mapatano ya JCPOA kwa madhumuni ya kupunguza athari haribifu za vikwazo vya upande mmoja vya Marekani na nchi za Ulaya kutofanya juhudi za kutosha katika uwanja huo licha ya kutoa ahadi chungu nzima zisizotekelezwa, ni jambo linalothibitisha kwa mara nyingine kwamba Tehran haina kosa lolote katika kudhihiri hali iliyopo sasa na kwamba ni nchi za Ulaya ndizo zimeshindwa au hazijataka kutekeleza majukumu na ahadi zao kwa Iran. Baada ya Marekani kujitoa katika mapatano ya JCPOA mnamo mwezi Mei 2018, Iran ilijitolea kutekeleza ahadi zake kwa muda wa mwaka mmoja na hatimaye ikaanza kupunguza taratibu uwajibikaji wake katika hatua tano, na hiyo ni baada ya nchi za Ulaya kuendelea kukiuka ahadi zao katika uwanja huo. Uchunguzi wa misimamo ya Ulaya baada ya Marekani kijitoa katika mapatano hayo unathibitisha wazi kwamba nchi za Ulaya zimeshindwa kabisa kutekeleza ahadi zao kwa Iran.
Nchi hizo zimekuwa zikidai kwamba kutokana na mapatano na JCPOA kuwa na nafasi muhimu katika kulinda usalama wa eneo na wa ulimwengu mzima, zitafanya hujudi zao zote kwa ajili ya kulinda mapatano hayo na kutekeleza ahadi zao katika uwanja huo. Pamoja na hayo lakini nchi hizo zimeshindwa kabisa kutekeleza ahadi hizo, na hasa kuhusiana na mfumo wa Instex, kutokana na mashinikizo ya Marekai na vilevile nchi hizo kutokuwa na nia thabiti katika uwanja huo. Kuhusu ukweli huo, Anna Sauerbrey, mwandishi wa Ujerumani anasema: Instex ni mfano wa wazi wa Ulaya kushindwa kuthibitisha stratijia yake huru mbali na Marekani.
Troika ya Ulaya pia ilichukulia hatua ya Iran kupunguza taratibu uwajibikaji wake katika mapatano ya JCPOA, hatua amabyo kwa hakika ilichukuliwa kutokana na nchi hizo tatu za Ulaya kutotekeleza ahadi zao, kuwa sababu ya kuikosoa na kuanza kutekeleza mchakato wa kurejesha vikwazo dhidi ya Tehran mnamo tarehe 14 Januari mwaka huu, ambapo zimeitaka Iran isimamishe mara moja mkondo huo na kurejea katika hali ya awali.
Suala jingine lilodaiwa karibuni na Borell ni kwamba bila ya mapatano hayo Iran ingeweza kuunda silaha za nyuklia. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa ripoti za mara kwa mara za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia, IAEA, Iran haijawahi kuelekeza mradi wake katika uundaji wa silaha za nyuklia bali daima imekuwa ikisisitiza kwamba mradi huo unatekelezwa kwa malengo ya amani. Kwa kuzingatia ukweli huo, badala ya Borell kuendelea kutoa maneno matupu na yasiyo na msingi kuhusu Umoja wa Ulaya na Troika ya Ulaya kuunga mkono mapatano ya JCPOA na kutoa ahadi zisizotekelezwa, ni bora achukue hatua za kivitendo katika uwanja huo na kuacha kushirikiana na Marekani dhidi ya Iran.