-
Jenerali Amir Hatami: Ushirikiano wa kijeshi wa Iran na Russia ni chanya
Aug 23, 2020 03:22Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Russia ni chanya na unaoendelea kuimarika.
-
Upinzani wa wanachama 13 wa Baraza la Usalama kwa ombi la Marekani la kuanzisha utaratibu wa "Snapback Mechanism"
Aug 22, 2020 05:57Kushindwa Marekani katika njama zake za kulazimisha kukubaliwa pendekezo la kuiongezea Iran muda wa vikwazo vya silaha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumeipelekea Washington kuchukua hatua ya kukurupuka ya kuwasilisha ombi la kuanzisha utaratibu wa kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran papo kwa hapo yaani "Snapback Mechanism." Ombi hilo la Marekani hata hivyo nalo limepingwa vikali ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
JCPOA na utaratibu wa "Snapback Mechanism", Marekani katika mkwamo wa Baraza la Usalama
Aug 21, 2020 22:26Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepinga hatua inayokiukaji sheria ya Marekani ya kutaka kutumia vibaya taratibu zilizowekwa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA za kurejesha upya vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.
-
Zarif: Serikali ya Trump imetengwa na kufedheheka tena katika medani ya kimataifa
Aug 21, 2020 06:38Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia upinzani wa jamii ya kimataifa dhidi ya hatua ya Marekani ya kutaka kutumia vibaya taratibu zilizowekwa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA za kurejesha upya vikwazo ilivyokuwa imewekewa Iran na kusema, kwa mara nyingine tena serikali ya Trump imetengwa na kufedheheka katika medani ya kimataifa.
-
Kupinga Umoja wa Ulaya hatua ya Marekani ya kutaka kutumia ‘Utaratibu wa Kifyatuo’
Aug 18, 2020 06:24Kushindwa kwa fedheha Marekani katika kupasishwa azimio ililopendekeza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuongezwa muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran kumeisukuma Washington na kuifanya ifikirie kutumia nyenzo nyingine kama utaratibu wa kusuluhisha mzozano katika JCPOA, unaojulikana kama "Utaratibu wa Kifyatuo", kwa kimombo "Trigger Mechanism".
-
Iran inaweza kujikidhia asilimia 90 ya mahitaji yake ya kijeshi
Aug 16, 2020 03:18Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hii inaweza kujikidhia asilimia 90 ya mahitajio yake ya kiulinzi kwa kiwango cha juu.
-
Kushindwa kifedheha Marekani katika kupitisha azimio dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama
Aug 15, 2020 21:45Tokea mwaka 2019, Marekani imekuwa ikifanya juu chini kuhakikisha kuwa Iran haiondolewi vikwazo vya silaha kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vikwazo hivyo vinapaswa kuondolewa Oktoba 2020. Pamoja na jitihada zake zote ambazo zimejumuisha vita vya kisiasa na kisaikolojia dhidi ya Iran na pia mazungumzo ya muda mrefu na wanachama wa baraza hilo, lakini hatimaye Marekani imefedheheka baada ya kushindwa vibaya sana.
-
Zarif: Wanaotumia vibaya mlipuko wa Beirut wanataka kuteteresha amani ya Lebanon
Aug 14, 2020 09:12Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran leo amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Waziri Mkuu wa Lebanon mjini Beirut na kusema kuwa, wanaotumia vibaya mlipuko mkubwa uliotokea katika bandari ya Beirut wana nia ya kuyumbisha amani ya Lebanon.
-
Iran: Uhusiano wa kidiplomasia wa Abu Dhabi na Tel Aviv ni ujinga wa kistratijia
Aug 14, 2020 03:37Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani hatua ya kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) na utawala wa Kizayuni wa Israel na kutaja hatua hiyo kuwa ni ujinga wa kistratijia ambao bila shaka utapelekea kuimarika mhimili wa muqawama na mapambano katika eneo.
-
Iran: Pompeo amelihadaa bunge la nchi yake ili kumuuzia silaha mwashamoto wa vita katika eneo
Aug 13, 2020 09:20Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amelihadaa bunge la nchi yake ili kuweza kumuuzia silaha mwashaji moto mkuu wa vita katika eneo hili la Asia Magharibi.