Iran inaweza kujikidhia asilimia 90 ya mahitaji yake ya kijeshi
(last modified Sun, 16 Aug 2020 07:48:17 GMT )
Aug 16, 2020 07:48 UTC
  • Iran inaweza kujikidhia asilimia 90 ya mahitaji yake ya kijeshi

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hii inaweza kujikidhia asilimia 90 ya mahitajio yake ya kiulinzi kwa kiwango cha juu.

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameyasema hayo leo mjini Tehran katika kikao na waandishi habari kwa mnasaba wa Siku ya Sekta ya Viwanda vya Ulinzi na huku akiashiria sifa za kipekee za sekta hiyo amesema: "Sisi tunajikidhia zaidi ya asilimia 90 ya mahitajio yote ya zana za kijeshi ambazo pia zinaundwa kwa viwango vya juu."

Ameongeza kuwa, pamoja na kuwepo vikwazo vya kimataifa na changamoto za kifedha lakini wataalamu Wairani wameweza kuunda zana za kiulinzi na hivyo nchi hii imeweza kujitoshelekeza katika sekta hiyo.

Amesema hivi sasa Iran inalenga kuwa nchi ya kwanza katika eneo kwa mtazamo wa sayansi na teknolojia na kwamba wataalamu wako mbioni kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.

Ndege ya kivita ya HESA Kowsar  ni kati ya ndege za kivita zilizoundwa kikamilifu nchini Iran

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameongeza kwa, katika kipindi cha miezi michache ijayo Iran itarusha satalaiti katika anga za mbali kwa kutegemea makombora yaliyoundwa humu nchini. Amesema kombora jipya la kubeba sataliti ambalo limeundwa Iran lina uwezo wa kubeba satalaiti iliyo na uzito wa zaidi ya kilo 100 na kuifikisha masafa ya juu katika anga za mbali zaidi ikilingnaishwa na sataliti zilizotangulia za Iran.

 

Tags